October 22, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Sekta ya afya Ilala kuboreshwa

Waziri wa Afya, Dr. Seif Rashid

Spread the love

MANISPAA ya Ilala, imekipandisha hadhi kituo za afya cha Pugu Kajiungeni kuwa hospitali. Lengo ni kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya Amana na kuokoa ya wananchi wanaofia njiani kutokana na kushindwa kupata huduma kwa haraka.

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Dk. Willy Sangu amesema, tayari hospitali hiyo imeanza kutoa huduma za kulaza wagonjwa na hivi sasa, wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha ujenzi wa chumba cha upasuaji na chumba cha kuhifadhi maiti.

Kubadilishwa kwa hospitali hiyo kumetokana na kazi za kitafiti zinazofanywa na taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Pugu Poverty Alleviation and Development Argency (PPADA); ambazo zimesaidia manispaa yake, kutambua matatizo ya zahanati na vituo vya afya vilivyopo katika maeneo ya pembezoni mwa manispaa ya Ilala.

PPADA ilisajiliwa 18 Februari 2003. Inafanya shughuli zake katika kata za Pugu, Kitunda, Gongolamboto, Chanika, Majohe, Msongola, Kivule na Ukonga.

Anasema kwa miaka miwili tangu PPADA imeanza shughuli zake, zahanati zimeboreshewa na wananchi wamepata imani kuwa fedha wanazotoa zinatumika vizuri kwa kuwa dawa wanapata na taarifa za kila robo ya mwaka zinatolewa kwao.

Taarifa hizo zinatolewa kwa njia ya mbao za matangazo.

Anasema, “Kwa sasa, tupo kwenye hatua za kujenga hospitali ya Kivule na Chanika… hii yote ni kusogeza huduma kwa wananchi.”

Mukurugenzi Mtendaji wa PPADA, Abraham Silumbu analishukuru Shirika la Foundation for Civil Society (FCS) kwa kufadhili mradi huo wenye gharama ya Sh. 135 milioni kwa miaka mitatu.

Anasema mradi wa kuboresha zahanati na vituo vya afya katika manispaa ya Ilala, ulianza mwaka 2011 na unatarajia kumalizika Agosti mwaka huu.

“Tumegundua kwamba lipo tatizo la utunzaji wa kumbukumbu hasa kwenye zahanati kote tulikopita tumeliona halafu wananchi hawapati taarifa sahihi za matumizi ya fedha zao.

“…Tumewahamasisha wananchi na tukawa tunawashirikisha kwenye utekelezaji wa majuku yetu na matokeo tuliwapa hadharani, hali imebadilika hivi sasa taarifa za kila robo ya mwaka zinawekwa kwenye mbao za matangazo,” anaeleza mkurugenzi huyo.

Anasema uwazi kwenye taarifa za fedha umeongezeka, watendaji kwenye zahanati wameongezeka na wananchi wamepata mwamko wa kufuatilia fedha zao.

Anasema mradi huo uliwashirikisha watendaji kuanzia ofisi mkurugenzi wa manispaa, mganga mkuu, watendaji wa kata na mitaa ambayo mradi huo ulihusika.

Katika robo ya kwanza ya utekelezaji wa mradi huo, mganga wa zahanati ya Mvuti alilazimika kukimbia kituo baada ya wananchi kubaini kuwa matumizi ya fedha hayapo sawa na ukosefu wa dawa ulichangia kupandisha hasira zao.

Anasema ilifika wakati mganga wa zahanati ya Mvuti aliwatishia kifo watendaji wa asasi ya PPADA kwa madai ya kumgombanisha na wananchi kiasi cha nyumba yake kutaka kuchomwa moto.

Mwandishi wa habari hii ni Irene Mark

error: Content is protected !!