Tuesday , 16 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Sekondari Ugombolwa, Migombani, Zawadi zaifurahia UBA Tanzania
Habari Mchanganyiko

Sekondari Ugombolwa, Migombani, Zawadi zaifurahia UBA Tanzania

Spread the love

TABIA ya kujisomea hujengwa, kwa kutambua hivyo Benki ya UBA Tanzania imekuwa ikishiriki kutoa mchango wa vitabu kuhakikisha inajenga tabia hiyo kwa wanafunzi nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Benki hiyo imekuwa ikitembelea shule mbalimbali na kutoa msaada wa vitabu kwa wanafunzi, katika kukabili tatizo la upungufu wa vitabu kwenye shule mbalimbali nchini.

Wiki iliyopita, benki hiyo ilitembelea shule kadhaa za sekondari Tabata, jijini Dar es Salaam kutoa msaada wa vitabu vya fasihi simulizi.

Shule za Sekondari zilizonufaika na ziara ya benki hiyo na kukabidhiwa vitabu vya fasihi ni pamoja na Shule ya Sekondari Ugombolwa, Migombani na Zawadi.

Miongoni mwa vitabu vilivyogawiwa ni pamoja na Things fall apart, The fishermen, The girl that can na Fine Boy. Vitabu hivyo vimeandikwa na wanafasihi mahiri akiwemo Chinua Achebe na Chigozie Obioma.

“UBA Tanzania imekua mstari wa mbele katika kusaidia ukuaji wa elimu Tanzania kwa kugawa vitabu kwenye shule za sekondari, pamoja na kuwezesha miundombinu katika sekta ya elimu,” amesema Asupya Nalingigwa ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Digitali.

Akizungumza wakati wa ugawaji vitabu Nalingigwa aliwaeleza wanafunzi umuhimu wa kutumia muda wao mwingi katika kujisomea badala ya kujikita kwenye mambo yasiyo muhimu kwao.

“Ni vema kutumia mitandao ya kijamii katika kujisomea na si katika mambo ambayo hayana manufaa kwenu. Jitahidini kutafuta mambo yenye tija katika maisha yenu ya baadaye,” alisema Nalingigwa.

Simon Machia, Mkuu wa Shule ya Ugombolwa ameeleza furaha yake baada ya Benki ya UBA Tanzania kukabidhi msaada wa vitabu shuleni kwake.

Amewaeleza wanafunzi wake kuenzi msaada huo kwa kujisoma kwa bidii kwa manufaa yao na jamii nzima.

“Ni muhimu kuenzi msaada huu kwa kujisomea ili hata hawa Benki ya UBA ijivunie kushiriki kuinua elimu kwa manufaa yetu kama nchi,” ameeleza mwalimu Machia.

Pia uongozi wa Shule za Migombani na Zawadi umeeleza furaha yao baada ya kupokea msaada wa vitabu hivyo kutoka UBA Tanzania.

Walimu wakuu wa shule hizo hawakusita kueleza changamoto zingine kwenye shule zao ikiwa ni pamoja na upungufu wa madarasa ya kusomea, viti, meza, madawati, kompyuta pamoja na uzio wa shule ili kuboresha usalama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Sekta binafsi yasifu utekelezaji wa Mkumbi

Spread the loveSERIKAL imepongezwa kwa utekelezaji wa mapendekezo ya sekta binafsi kupitia...

Habari Mchanganyiko

Kamati ya bunge yapigia chapuo kilimo ikolojia

Spread the loveSERIKALI kupitia Wizara ya Kilimo imeshauriwa kushirikiana na wadau wa...

Habari Mchanganyiko

Serikali yapata hasara 113 milioni hospitali kuwapa misamaha wagonjwa wasiostahili

Spread the loveSERIKALI imepata hasara ya kiasi cha Sh. 111.76 milioni, baada...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

error: Content is protected !!