January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Segerea waanza kukabili changamoto za Elimu

Spread the love

TAASISI binafsi na wadau wa elimu nchini, wametakiwa kuiunga mkono Serikali katika juhudi za kutekeleza mkakati wa elimu bure, kutokana na matatizo yanayoikabili sekta hiyo ikiwemo madawati na vyoo kwenye baadhi ya shule. Anaandika Josephat Isango … (endelea).

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Mbunge wa Segerea, Bonny Kaluwa (CCM), wakati wa kuzindua Kampeni ya Mazingira Bora kwa Elimu Bora inayohitaji takribani sh.bilioni tisa ili kufanikiwa.

Mbunge huyo aliweka bayana kuwa kampeni hiyo imezinduliwa kwa ajili ya shule za Segerea, ambayo bado ina matatizo ya miundombinu ya kielimu ikiwemo visima vya maji, matundu ya vyoo vya kisasa, madawati na majengo ya shule.

Ameongeza kuwa hatua hiyo inalenga kuisaidia na kuikomboa jamaii katika sekta ya elimu ili kuhakikisha inasaidia kufuta ujinga, ambapo utekelezaji wake utakuwa na maboresho. “Ili kukabiliana na suala hilo katika Kata 13 za Segerea zote kuna shule, hivyo inahitajika madawati 15,000, matundu ya vyoo vya kisasa 1335, visima vya maji 12 na vyumba maalum vya watoto wa kike 38,”alisema.

Kaluwa alisema kuwa kampeni hiyo ni mwendelezo wa kampeni iliyowahi kufanyika katika kata ya Kipawa kwa kusimamiwa na mfuko wa elimu wa ‘Bonnah Education Trust Fund’, mnamo mwaka 2011.

“Kampeni hii…itadumu kwa miezi sita, lakini ili kufanikisha kampeni hiyo itawahusisha wadau mbalimbali wa elimu waliopo ndani na nje ya Segerea kama vile Serikali, Makampuni, Mashirika na watu binafsi,” amesema.

Mratibu wa mpango huo, Shamshudin Ahmed alisema kuwa kampeni hiyo itaambatana matembezi ya hiyari Februari 2, mwaka huu ili kuwashirikisha wadau wa elimu kuchangia mpango huo.

“Inatakiwa tuisadie serikali katika mkakati wake, kwani haipaswi kila kitu tukaichia hali ya kuwa vingine tuna uwezo wa kuvifanya ikiwemo kuchangia madawati na huduma ya maji kwa wanafunzi wetu,” amesema

error: Content is protected !!