January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sefue: Watendaji serikalini kumbukeni wajibu wenu

Balozi Ombeni Sefue

Spread the love

KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amewataka watendaji wakuu wa serikali kutimiza wajibu wao katika kufanikisha uchaguzi mkuu ujao. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Ametoa angalizo hilo leo wakati akifungua mkutano wa faragha wa makatibu wakuu, manaibu makatibu wakuu na makatibu tawala wa mikoa mjini hapa.

“Wajibu huu ni mkubwa, ni wajibu unaotuhusu sote, na lazima tuutekeleze inavyopasa na kwa ukamilifu, kwa maslahi na manufaa ya taifa letu,” amesema.

Amesema, watendaji wakuu wana dhamana kubwa katika kufanikisha uchaguzi mkuu na kwamba, kila mmoja atambue hilo na ashiriki kikamilifu katika mada zitakazowakilishwa.

Amesema, kila mmoja anapaswa kuzijua sheria, taratibu na kanuni zinazohusu uchaguzi mkuu pamoja na kujua namna ya kuendesha shughuli za serikali katika kipindi hiki.

Aliyataja baadhi ya masuala muhimu ya kuzingatia ni yale yanayohusu ulinzi na usalama wa nchi na pia mkutano uwasaidie kupata maoni na ushauri wa namna bora ya kuipokea serikali ya awamu ya tano ili ianze kazi kwa haraka na kwa ufanisi.

Ametaja mada zitakazowasilishwa katika mkutano huo kuwa ni pamoja na maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na hali ya ulinzi na usalama kuelekea uchaguzi huo.

Pia matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kuboresha utendaji wa serikali 2015 na waraka wa mkuu wa utumishi wa umma Namba 1. wa mwaka 2015 kuhusu utaratibu kwa watumishi wa umma wanaogombea nyadhifa za kisiasa nchini.

Pia katika mkutano huo Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kitawasilisha mada ya ‘nafasi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Mitaala yake katika kuwaandaa viongozi.’

Amesema, changamoto zitakazoelezwa katika mada ya ulinzi na usalama wa nchi zitasaidia kutujenga kimkakati zaidi katika kipindi ambacho kumejengeka katika jamii tabia na utamaduni wa kuvunja, kutojali na kutotii sheria.

Balozi Sefue amewaagiza kurejea mada ya ‘nafasi ya Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015’ iliyotolewa kwenye mkutano wa mwaka jana ambayo ilibainisha wazi majukumu ya watendaji wakuu na ya kila taasisi inayohusika.

Kaulimbiu ya mkutano huo inasema ‘Nafasi na wajibu wa watendaji wakuu wa serikali kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2-015 na kuingia madarakani serikali ya awamu ya tano’ inayolenga kuwakumbusha watumishi wa umma na watendaji wakuu nafasi na wajibu wao katika kufanikisha uchaguzi Mkuu.

error: Content is protected !!