July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sefue: Mchakato wa vitanda haukuanzia bungeni

Spread the love

KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amesema mchakato wa kununuliwa vitanda katika hospitali ya Taofa ya Muhimbili, haukuanza mara baada ya kauli ya Rais John Magufuli. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Balozi Sefue alilazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya wananchi kuhoji imewezekanaje, mchakato wa manunuzi ya vitanda hivyo ufanikiwa ndani ya siku moja baada ya Rais kutoa kauli hiyo.

Rais Magufuli aliamuru Sh. 250 milioni zitumike kununua vitanda hivyo, kutoka katika michango ya wabunge wa CCM zilizochangwa kwa ajili ya sherehe ya kupongezana ambazo zilikuwa Sh. 265 milioni.

Barozi Sefue amesema kuwa uwamuzi wa kupunguza gharama za sherehe za kuwapongeza wabunge ulianza mapema na hata utaratibu wa utekelezaji pia ulianza mapema na kuwa alichokifanya Rais Magufuli bungeni ni hitimisho tu.

Amesema jambo muhimu ni kuwa wananchi wanatakiwa kutambua kuwa tatizo halikuwa ni vitanda tu bali hata sehemu ya kuviweka vitanda hivyo, hivyo walilazimika kufanya maandalizi ya kulitumia jengo la Taasisi ya Mifupa (MOI) ambalo bado halijakabidhiwa rasmi na wakandarasi.

Balozi Sefue alitumia ziara hiyo kukagua vitanda hivyo pamoja na ukarabati vifaa tiba vikiweno mashine za MRI na CT-Scan ambazo ziliharibika tena baada ya kufanyiwa matengenezo kwa mara ya kwanza.

Hospitali hiyo imekabidhiwa jumla ya vitanda 300, magodoro 300, viti maalum vya wagonjwa (Wheel chairs) 30, vitanda maalum vya kubebea wagonjwa (Stretchers) 30, shuka 1,695 na mablanketi 400 ambavyo vimegharimu jumla ya Sh. 251 milioni.

error: Content is protected !!