October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sauti Sol yatishia kushitaki kampeni za urais za Raila Odinga

Spread the love

 

KUNDI la muziki kutoka nchini Kenya , linalofahamika kwa jina la Sauti Sol, limetishia kushitaki kampeni za urais za Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga, kwa madai ya ukiukaji wa hakimiliki. Anaripoti Rhoda Kanuti kwa msaada wa Mashirika ya Kimataifa … (endelea).

Taarifa hiyo imekuja baada ya akaunti za mitandao ya kijamii za Odinga,zinasemekana kutumia wimbo wa Sauti Sol wa Extravaganza wakati wa kumtambulisha, Martha Karua kama mgombea mwenza wa Muungano wa Azimio la Umoja.

Katika taarifa iliyochapisha kwenye mtandao wa Twitter na kikundi hicho cha Sauti Sol wakilalamika kuhusu matumizi ya muziki wao, katika kampeni zinazoendelea za kisiasa nchini humo.

Walisema ‘’hawakuwa na uhusiano wala kuhusishwa katika kampeni ya Azimio la Umoja au vuguvugu lolote la kisiasa au chama.’’

‘’Tumesikitishwa na kampeni ya Azimisho la Umoja ya kupuuza waziwazi haki yetu ya kudhibiti matumizi ya hakimiliki yetu.’’

Hata hivyo chama hicho cha ODM ambacho ni sehemu ya muungano wa Azimio ,ambaye Odinga nimshiriki, kilisema kuwa wanathamini muziki wa Sauti Sol,’’kucheza wimbo wao ilikuwa ni kuonesha mapenzi kwa kazi yao.’’

Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa kijamii,wameitupia lawama bendi hiyo, wakisema kwamba muungano wa Odinga ulikuwa umelipa Chama cha Hakimiliki ya Muziki Kenya (MCSK) zaidi ya ada ya leseni ilitumia kazi za muziki zilizo na hakimiliki katika kampeni yao.

Pia MCSK nichombo cha serikali kinachosimamia ulipaji wa mirabaha kwa wasanii nchini humo.

Aidha wasanii wengi wakiwemo Souti Sol, wamekikosoa chombo cha hakimiliki juu ya muundo wanaotumia kuwafidia, pia Sauti Sol ni moja ya kubwa barani Afrika na ilishinda Tuzo za Muziki za MTV Afrika mwaka 2016.

error: Content is protected !!