June 19, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Sauti hii imfikie Rais Magufuli

Spread the love

MAHMUDU Abdul Nondo, Naibu Waziri wa Mikopo katika Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) amesema ni wakati muafaka kwa Rais John Magufuli ambaye amejipambanua kama rais wa masikini na wanyonge kujitokeza na kusitisha mateso ya wanafunzi wa vyuo vikuu, wakiwemo yatima waliokosa mikopo, anaandika Charles William.

Akizungumza katika kipindi cha Hotmix ambacho hurushwa na kituo cha runinga cha EATV, Mahmudu amesema licha ya wanafunzi wengi kukidhi vigezo vya kupata mikopo vilivyotangazwa na serikali kwa mwaka masomo 2016/2017 lakini bodi ya mikopo ya elimu ya juu imewanyima mikopo hiyo.

Amemsihi Rais Magufuli, kuingilia kati suala hilo haraka kwani wanafunzi waliokosa mikopo ni masikini na yatima na kwamba, kwa kuwa serikali ya awamu ya tano imekuwa ikisifika kwa kukusanya kodi hivyo haiwezi kushindwa kuwapa mikopo wanafunzi hao.

Msikilize zaidi……

error: Content is protected !!