Monday , 26 February 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa ‘Saudi Arabia imekiri kushindwa’
Kimataifa

‘Saudi Arabia imekiri kushindwa’

Adel al-Jubeir, Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia
Spread the love

NAIBU Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sheikh Naim Qassim amesema kuwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia inaonesha kukiri kushindwa kwake baada ya kukubali kuanzishwa maeneo ya kupunguza mivutano nchini Syria, anaandika Jovina Patrick.

Jumapili ya jana Adel al-Jubeir, Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia akizungumza na waandishi wa habari nchini humo ikiwa ni miaka sita ya vita na baada ya kushindwa makundi ya kigaidi kwa ajili ya kuiondoa madarakani serikali ya Damascus, alisema kuwa Saudia inakubaliana na pendekezo la kuanzishwa maeneo ya kupunguza mizozo nchini humo.

Lengo kuu la mazungumzo hayo ni kutiwa saini makubaliano yenye lengo la kuanzishwa maeneo ya kupunguza migogoro nchini Syria. Kufuatia hali hiyo Sheikh Naim Qassim akizungumza na kanali ya televisheni ya al-Manar amesema kuwa, Saudia inapitia wakati na kipindi kigumu kutokana na kushindwa mipango yake yote katika eneo la Mashariki ya Kati.

Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, muqawama nchini Syria umekuwa ukisajili ushindi na kwamba ushindi huo utaendelea

Ameongeza kuwa, kukombolewa mji wa Aleppo kumefelisha njama za maadui za kutaka kuigawa vipande nchi ya Syria na kwamba kukombolewa mji wa Deir ez-Zor, ni ushindi mwingine mkubwa dhidi ya genge la kigaidi la Daesh.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wanajeshi Ukraine waishiwa risasi, 31,000 wauawa

Spread the loveRais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amesema zaidi ya wanajeshi 31,000...

Kimataifa

Waziri mkuu Palestina ajiuzulu

Spread the loveWaziri Mkuu wa Palestina, Mohammed Shtayyeh ametangaza kujiuzulu pamoja na...

Kimataifa

Rais mstaafu ahukumiwa miaka 4 jela

Spread the loveMahakama ya mjini Tunis imemhukumu rais wa zamani wa Tunisia,...

Kimataifa

Malawi yaondoa vikwazo vya viza kwa nchi 79 ikiwamo TZ

Spread the loveWaziri wa usalama wa ndani nchini Malawi, Ken Zikhałe ametangaza...

error: Content is protected !!