Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sare, mafunzo askari kutafuna Bil. 34.7/-
Habari za Siasa

Sare, mafunzo askari kutafuna Bil. 34.7/-

Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni
Spread the love

 

WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi imeweka kipaumbele kwa mafunzo na ununuzi wa sare za askari ambapo jumla ya Sh 34.7 bilioni zimetengwa kwa kazi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma …(endelea)

Hayo yameelezwa leo Alhamisi tarehe 5 Mei, 2022 bungeni jijini Dodoma na Waziri, Hamad Masauni wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti yam waka 2022/2023.

Waziri huyo amesema jumla ya Sh. 18.1 zimetengwa kwenye bajeti ya mwaka 2022/2023 kwa ajili ya ununuzi wa sare huku mafunzo ya askari yakitengewa Sh. 16.6 bilioni.

Masauni amesema kwa muda mrefu kumekuwa na changamoto ya upungufu wa sare za askari,“Mheshimiwa Rais, Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuimaliza changamoto hii kwa askari wetu.”

Amefafanua zaidi kuwa fedha za sare hizo Shilingi 11.7 bilioni ni kwa ajili ya Jeshi la Polisi, Sh 4.1 bilioni za Jeshi la Magereza, Sh. Bilioni moja kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Sh. 1.3 bilioni kwa ajili ya Idara ya Uhamiaji.

“Natumia fursa hii kuyaelekeza Mashirika ya Uzalishaji Mali ya Jeshi la Polisi na Magereza kuanza mchakato wa kushiriki zabuni kwa ajili ya ununuzi wa sare za vyombo vyote vya usalama vilivyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,” amesema.

Amesema zabuni hizo kwa majeshi ni kutimiza matakwa ya Amiri Jeshi Mkuu ya kuyawezesha mashirika hayo kujiimarisha kiuchumi pamoja na kuhakikisha vyombo vya usalama vinanunua sare zenye ubora, viwango na kwa gharama nafuu.

Kwa upande wa mafunzo Masauni amesema kwa muda mrefu maafisa na askari wa majeshi yote yaliyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi walikuwa wakichangia gharama wanapohudhuria mafunzo, hivyo kuathiri hali za maisha ya familia zao na askari wetu wanapokuwepo mafunzoni.

“Ninayo furaha kulitangazia Bunge lako kuwa katika mwaka 2022/2023, jumla ya Sh. 16.6 zimetengwa kwa ajili ya kugharamia mafunzo ya maafisa, wakaguzi na askari.”

Amesema kati ya fedha hizo Sh. 11.6 bilioni ni kwa ajili ya Jeshi la Polisi, Sh. 3.5 bilioni za Jeshi la Magereza, Sh. 555 milioni kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Sh. 900 milioni kwa ajili ya Idara ya Uhamiaji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

error: Content is protected !!