September 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Sangoma wapandishwa kortini

Spread the love

WATU watatu wanaosadikika kuwa waganga wa kienyeji wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa la kosa utapeli, anaandika Faki Sosi.

Watu hao ni Halid Mjewa (55), Salum Mwawala (24) na Said Magand (28).

Akisoma mashtka hayo Nassoro Katuga, mbele ya Magreth Bankika, Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo amesema, kwa waakati tofauti mwaka 2012 katika eneo lisilojulikana kwa pamoja walijipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Katuga amedai kuwa, kati ya mwezi Januari hadi Desemba 2012 eneo la Kibamba, Kinondoni jijini Dar es Salaam walidanganya na kijipatia kiasi cha Sh. 260 milioni kutoka kwa Sophia Lolila kwa kujifanya waganga na kudai watamsaidia kwa nguvu za giza aolewe, kupata watoto na biashara yake ya mbao itaenda vizuri.

Katuga amesema kuwa, upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kwamba, kesi hiyo itajwe kwa usikilizwaji wa awali.

Washtakiwa wote wamekana mashitaka hayo. Dhamana ya washitakiwa ipo wazi kwa mashrti ya kila mmoja awe na wadhamini wawili na kusaini hati ya dhamana ya Sh. 43.3Milioni kila mmoja.Kesi itatajwa tena Julai 4 Mwaka huu.

error: Content is protected !!