October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sangoma aliyetabiri kifo cha Malkia Elizabeth aibua mjadala

Spread the love

 

WAKATI dunia ikiomboleza kifo cha Malkia Elizabeth II wa Uingereza, watumiaji wa mtandao wa Twitter wameibua Tweet ya mganga mmoja matata aliyebashiri kifo cha Malkia Elizabeth mwaka mmoja uliopita.

Mganga huyo kupitia Twitter yake amejieleza katika utambulisho wake kwamba yeye ni mtaalamu wa ubashiri kutumia ushirikina. Anaripoti Felister Mwaipeta, TUDARCo … (endelea).

Malkia alifariki Septemba 8 na Tweet ya mganga huyo aliyefahamika kwa jina Orunmila inaonesha kwamba alipiga ramli na kutoa ubashiri wake kuhusu kifo cha Malkia kwamba kingetokea tarehe kama hiyo.

Ubashiri wake unaonekana kwenye Tweeter iliyotolewa tarehe Agosti 24 mwaka jana.

Baada ya ubashiri huo kutimia kwa kifo cha malkia, sasa Orunmila amejitanua kifua na kutamba kwamba kwa ubashiri wake.

“Malkia wa Uingereza atafariki dunia tarehe 8 Septemba. Mimi naona tarehe hii ikimzingira juu ya kichwa chake. Wewe endeleea kutoniamini lakini utaona,” mganga huyo aliandika mwaka jana Agosti kwa lugha ya Kifaransa.

Aidha, baada ya ubashiri wake kutimia, mshirikina huyo alirudi kwenye Twitter na kujitapa kwamba kazi yake ubashiri si ya kubahatisha kwani huwa anabashiri na tofauti huwa ni kidogo.

Alisema kwamba katika ubashiri wake mwaka jana, asingeweza kubashiri kwa sahihi muda na chanzo cha kifo cha malkia Elizabeth.

“Hatuwezi kutenda au kushawishi, kutabiri tu, kujua mapema na wakati mwingine tofauti ni kidogo. Hapo sikuweza kujua saa wala sababu ya kifo,” mganga Orunmila aliandika.

error: Content is protected !!