MBUNGE wa jimbo la Makete nchini Tanzania, Festo Sanga, amemwomba Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia katika suala la uagizaji mbolea kutokana na kukwamishwa na wanasiasa na watendaji wa Serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Mbunge huyo amesema suala la mbolea Rais Samia ameweka Sh. 150 bilioni kwaajili ya ruzuku ya mbolea lakini changamoto imekuwa kwenye mfumo wa uagizaji wa pamoja.
Amesema Waziri wa Kilimo ameanza kurekebisha mfumo wa uagizaji wa pamoja kwasababu uliopo sasa unamufaisha mwagizaji mmoja.
“Pamoja na jitihada za Waziri yapo mambo ya siasa yanafanywa na wanasiasa na watendaji wa Serikali kukwamisha jambo hili, naomba Rais aingile kati jambo hili kwasababu mbolea inahitajika kila mahali,” amesema Sanga.
Leave a comment