January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sanders, Trump wasonga mbele

Spread the love

DONALD Trump wa Chama cha Republican na Bernie Sanders wa Chama cha Democratic wanasonga mbele baada ya ushindi walioupata katika mchujo wa Jimbo la New Hampshire. BBC.

New Hampshire ndilo jimbo la tatu kuandaa mchujo baada ya mchujo wa Iowa kufanyika wiki iliyopita. Ted Cruz (Republican) na Bi Hilary Clinton walishinda mchujo huo wa Iowa.

Matumaini yao yanaelekezwa kwenye Jimbo la Sotuh Carolina na Nevada nchini Marekani. Wakati Sanders akiwa na matumaini ya kupitishwa na chama chake dhidi ya mpinzani wake Hillary Clinton, Trump anarejesha matumaini yake kupitia Republican.

Kwa upande wake, Sanders anaamini kwamba Wamarekani wanamtaka kwa kuwa wanahitaji mabadiliko. Hii ni kampeni ndani ya chama chake dhidi ya Clinton anayeonekana kuwa mpinzani wake wa karibu.

Imekuwa kawaida kwa Sanders na yule wa Republican, Trump kushawishi wapiga kura kuchagua watu ambao wapo tayari kwa mabadiliko, wanaposema hivyo wanajionyooshea kidole wao wenyewe.

Mchujo huo wa New Hampshire umewapa washindi nguvu mpya wanapoelekea kwa michujo ijayo South Carolina na Nevada.

Lakini pia ushindi wa Trump New Hampshire ndio wa kwanza mfanyabiashara huyo kutoka New York, ambaye hajawahi kuwania wadhifa wowote wa siasa katika maisha yake.

Ratiba ya mikutano inayoendelea ni kama ifuatavyo:-

20 Feb: Mikutano ya Nevada (Democratic), Uchaguzi wa South Carolina (Republican)

23 Feb: Mikutano ya Nevada (Republican)

27 Feb: Uchaguzi wa South Carolina (Democratic)

Machi:

Majimbo 13 hupiga kura Jumanne kuu ikiwa ni pamoja na majimbo sita Kusini. Ni nafasi nzuri kwa mgombea kujithibitishia ubabe, ingawa bado mambo huwa yanaweza kubadilika baadaye.

1 Machi:¬†Jumanne Kuu’: Mikutano ya Alabama, Arkansas, Georgia, Massachusetts, Oklahoma, Tennessee, Texas, Vermont, Virginia Primaries; Alaska & Wyoming (Republican), Colorado Caucuses (Democratic)

5 Machi: Mikutano ya Kansas, Uchaguzi Louisiana, Mikutano Kentucky & Maine (Republican), Mikutano Nebraska (Democratic)

6 Machi: Mikutano ya Maine (Democratic)

8 Machi: Mikutano ya Hawaii & Idaho (Republican), Uchaguzi wa Idaho (Republican), Michigan & Mississippi

15 Machi: Uchaguzi wa Florida, Illinois, Missouri, North Carolina, Ohio

Kuna majimbo makubwa ambayo yatakuwa yakipigania mwezi Machi, hasa majimbo ambayo mshindi hupokea wajumbe wote. Pia kuna majimbo yasiyo na msimamo mkali ambako kuna uwezekano mkubwa kwa wagombea kuwashawishi wapiga kura kubadili msimamo.

22 Machi: Uchaguzi Arizona, Mikutano Utah, Mikutano Idaho (Democratic)

error: Content is protected !!