August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sanchez apata ‘dili’ nono China

Alexis Sanchez

Spread the love

LICHA ya Arsenal kumpa ofa nono ya pauni laki mbili, Alexis Sanchez kwa wiki kama akikubali kuongeza mkataba wake ambao umebakisha miezi 18, lakini kiungo huyo amepata ofa kutoka kwenye moja ya klabu inayo shiriki Ligi Kuu  China na kumtengea kiasi cha pauni laki nne kwa wiki.

Klabu hiyo ambayo inasemekana ipo tayari kumlipa kiasi hicho cha pesa kama mshambuliaji huyo atashindwa kuongeza mkataba na klabu yake ya sasa kwa kushindwa kulipwa kiasi cha mshahara atakachotaka ambacho mpaka sasa kocha Arsen Wenger hayupo tayari kumlipa.

Si mara ya kwanza kwa klabu za China kufanya sajiri za wachezaji wenye majina makubwa na kuwalipa mishahara mikubwa kama Samuel Eto’o, Ezequiel Lavezz, Graziano Pele na Nicolas Anelka huku wakiwa na lengo la kukuza soka katika nchi yao.

Sanchez ambaye anahusishwa kuondoka katika klabu hiyo katika dirisha dogo la usajiri kutokana na kukataa ofa iliyowekwa mezani na klabu yake ya Arsenal na kutaka kulipwa zaidi Dola laki 290,000 kwa wiki huku wakala wake anahusishwa kufanya mazungumzo na Pep Guardiola ambaye anakinoa kikosi cha Manchester City.

Mshambuliaji huyo ambaye kwa sasa anamchango mkubwa sana ndani ya kikosi cha Arsenal ambapo mpaka sasa amefunga jumla ya mabao 11 katika michezo ya ligi kuu na kuwa kinara wa ufungaji sawa na mshambuliji wa Chelsea, Diego Costa ambao wamefungana kwa mabao.

error: Content is protected !!