Monday , 29 May 2023
Home Habari Mchanganyiko Sanaa ya ufundi yapigiwa chapuo
Habari Mchanganyiko

Sanaa ya ufundi yapigiwa chapuo

Adrian Nyangamale, Rais wa Mradi wa Utambuzi wa Wasanii za Sanaa ya Ufundi (TAFCA)
Spread the love

NAJIMA Giga, Mwenyekiti wa Bunge ewataka watendaji kutambua sanaa ya ufundi, inayofanywa na wasanii ili kuongeza ajira kwa vijana. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mwenyekiti huyo ametoa kauli hiyo wakati akifungua semina ya utambuzi wa sanaa ya ufundi, iliofanyika katika ukumbi wa Cathedral uliopo jijini Dodoma.

Amesema, sanaa ni jambo zuri na linapaswa kuheshimiwa na kila mtu ili kuinua sekta hiyo ambayo inaachwa nyumba na wadau mbalimbali.

Giga amesema, lengo la kufanya hivyo ni pamoja na kutambua umuhimu wa wasanii ili nao waweze kusonga mbele katika kazi zao za kila siku.

Amesema, wasanii ni watu muhimi katika jamii yetu kwa sababu wanafanya vitu ambavyo vinasaidia kuelimisha jamii kwa ujumla.

Godfrey Ngereza, Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa amesema, kuna kila sababu ya kulisimamia suala hilo ili sana’a ya ufundi itambulike.

Ngereza amesema, wao kama baraza wako mstari wa mbele kutoka elimu kwa watu ili wajue umuhimu wa sanaa kwa ujumla.

Amesema, baada ya semina hiyo, wana imani watendaji watakuwa mstari wa mbele kuhakikisha sanaa inasonga mbele kwa kila msanii.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Kirigini kuzikwa leo Butiama

Spread the love  MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Musoma Vijijini (1980-1985), Herman...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jeshi la Polisi kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika utafiti

Spread the love  JESHI la Polisi Nchini limesema kuwa katika kukabiliana na...

Habari Mchanganyiko

Kampeni ya Samia Legal Aid yazinduliwa Manyara, kesi 45 zapokelewa

Spread the love  KAMPENI ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, imezinduliwa...

Habari Mchanganyiko

NMB ya kwanza kuzindua Malipo kwa QR na UnionPay International

Spread the loveBENKI ya NMB kwa kushirikiana na UnionPay International (UPI), wamezindua...

error: Content is protected !!