July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Samwel Sitta akatwa Uspika

Spread the love

MKONGWE wa siasa ambaye aliyekuwa Spika wa bunge la tisa, Samuel Sitta ambaye alikuwa wakiwania nafasi ya uspika katika Bunge la 11, Kamati Kuu ya (CCM) imelikata rasmi jina lake licha ya kufanya kampeni mapema juzi kwenye viwanja vya Bunge. Anandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Akitangaza majina yaliyopitishwa na kamati kuu Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema katika halmashauri hiyo imeyapitisha majina matatu ambayo ni Job Ndugai, Abdullah Ally Mwinyi na Tulia Akson.

Nape amesema kesho saa nne asubuhi majina hayo yatapelekwa yawasilishwa kwa wabunge wa CCM kwa ajili ya kupitisha jina la mgombea mmoja ambaye atagombea nafasi hiyo na wakambi ya upinzani.

Nafasi za Unaibu Spika

“Kwa bahati mbaya jana kwa makosa tulieleza ratiba ambayo ilikuwa inazungumza kwamba suala la naibuNaibu Spika lingeshughulikiwa leo na kamati kuu, kwa mujibu wa kanuni za Chama cha Mapinduzi zinaeleza suala la Naibu Spika halishughulikiwi na kamati kuu,” amesema.

Alifafanua kuwa suala la Naibu spika linashughulikiwa na kamati ya wabunge wa CCM.

“Kwa mujibu wa kanuni ya kanuni za kamati ya wabunge wote wa CCM, toleo la 4, 2011 ibara ya 57, “Inasema mwanachama wa CCM anayetaka kugombea nafasi ya Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano atajaza fomu maalum ya maombi na kuiwasilisha kwa katibu wa kamati ya wabunge wote wa CCM,…

“Kwa muda uliowekwa na ada ya fomu itakuwa Sh. 100,000, ambazo zitalipwa wakati mgombea anarudisha fomu kwa katibu wa kamati,” amesema Nape.

Aidha alifafanua kuwa suala la mgombea unaibu spika ni suala ambalo linamalizwa na kamati ya wabunge wa CCM.

Amesema kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Ofisi ya kamati ya wanbunge wa CCM, wanaotaka kugombea nafasi hiyo watachukua fomu kuanzia Novemba 16 na kurudisha Novemba 17 kabla ya saa 10 jioni.

Katibu huyo alisema, uchaguzi utafanywa na wabunge wa CCM Novemba 17 kwa kumpa mgombea mmoja atayegombea nafasi ya unaibu wa spika kupitia tiketi ya CCM.

Amesema majina hayo ya makada wa CCM yatapelekwa kwenye kamati ya wabunge wa CCM leo kwenda kuchaguliwa jina mmoja ili awe mgombea wa Uspika wa Bunge.

Nape alisema majina hayo yatawsilishwa kwenye kikao kitakachofanyika leo saa nne asubuhi katika ukumbi wa White House ambapo yatapigiwa kura na kupata jina moja.

Majina hayo matatu yametokana na majina 21 ya makada waliojitosa katika kinyang’anyiro cha spika wa Bunge.

Kati ya wanaCCM hao 21 waliogombea, kada mmoja hakuweza kurudisha fomu na hivyo kufanya idadi ya wagombea waliojadiliwa na CC kubaki 20.

Mgombea ambaye hakurejesha fomu hiyo ni aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Itali, Costa Mahalu.

Miongoni mwa makada walijitosa kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo ni pamoja na mwanasiasa mkongwe na aliyewahi kuwa spika wa Bunge la tisa, Samweli Sitta, aliyekuwa naibu spika wa bunge la kumi, Job Ndugai, Tulia Akson na Abdullah Mwinyi, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Itali, Costa Mahalu.

Wengine ni Rita Mlaki, George Nangale, Dk, Medard Kalemani, Julius Pawatila, Agnes Makune, Mwalika Watson,Dk, Kalokola Muzamil, Didas Masaburi, Simon Rubugu, Veraikunda Urio, Gosbert Blandes, Banda Sonoko na Leonce Mulenda.

Alipotafutwa mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo Samuel Sitta ili kutoa maoni yake kuhusu kukatwa jina lake alisema alikuwa hajapata taarifa hizo.“Siwezi kukatwa itakuwa wanafanya mchezo hata hivyo itabidi nisubiri nielezwe kasoro hizi na zile basi,”alisema Sitta.

Hata hivyo, Sitta, alisema hawezi kukadiria kitu asichokijua itabidi asubiri aitwe na kuelezwa sababu zilizofanya akatwe.

Akizungumzia kauli yake ya kwenda mahakamani kama angekatwa, Sitta alisema kuwa atakwenda mahakamani kama atakuwa ameonewa katika kukatwa huko.

error: Content is protected !!