November 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Samia: Wananchi jipindeni kufanya kazi

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Watanzania kujipinda kufanya kazi ili mapato yapatikane kusukuma gurudumu la maendeleo ya Taifa hasa ikizingatiwa mapato yayanayopatikana ni madogo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Samia ametoa rai hiyo leo tarehe 22 Novemba, 2022 aliposimama kuzungumza na wananchi wa Kondoa – Dodoma wakati akielekea Manyara na Arusha.

Amesema hakuna kazi zilizosimama na kazi inaendelea kwenye sekta zote Tanzania

“Tunaomba wakati serikani inajipinda kufanya kazi wananchi nanyi jipindeni kufanya kazi, anayelima alime, anayevua avue, anayechimba achimbe wote tufanye kazi tupate mapato nchi yetu iende mbele, nchi yetu ni kubwa lakini mapato ni madogo ila hayohayo tunayopata tunagawana hapa na pale,” amesema.

Amesema Serikali imejitahidi kushusha fedha kwa wananchi na katika sekta mbalimbali na huo ndio mwenendo Serikali hiyo anayoiongoza kwa sasa.

“Mwananchi kwanza sisi huku juu baadae… tutajijua tutakavyoishi. Ndio maana tunashusha fedha nyingi zije zitoe huduma kwa wananchi,” amesema.

error: Content is protected !!