October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Samia: Walioiba pembejeo ruzuku nataka wazione rangi zangu

Spread the love

RAIS SamiaSuluhu Hassan ameiagiza Taasisi yaKuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) “kuwashughulikia kisawasawa” wezi wa pembejeo za ruzuku na fedha za vyama vya ushirika waliokamatwa mkoani Simiyu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Ametoa maagizo hayo leo Jumatatu tarehe 4 Aprili 2022 jijini Dodoma wakati akizindua ugawaji wa vitendea kazi kwa maafisa ugani wa kilimo.

“Wakuu wa mikoa nimeona kwenye habari Mkuu wa Mkoa Simiyu amekamata watu wanaoiba pembejeo za kilimo za ruzuku na hili liko TAKUKURU naomba wazisome zile rangi zangi, nataka washughulikie kisawasawa ili iwe fundishokwa wengine wasiibe na waziri mkuu usimamie hilo,” amesema Rais Samia.

Amesema mwaka jana alielekeza kufanya majaribio ya kutoa ruzuku za pembejeo kwa wakulima na yameonesha mafanikio makubwa.

“Tumepata matokeo mazuri kwenye pamba, nimeelekeza sasa kuwe na mfuko maalum wa pembejeo. Mwaka jana tulitumia Sh 56 Bilioni kwenye pamba, Sh. 61 bilioni kwenye korosho na Sh 32 bilioni kwenye tumbaku. Matokeo kiwanda cha tumbaku Morogoro tunakifungua kwasababu tumbaku imeongezeka.”

error: Content is protected !!