Monday , 30 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Samia: Sijaumbwa kufokafoka
Habari za Siasa

Samia: Sijaumbwa kufokafoka

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema atafanya kazi kwa kalamu na hata siku moja hatomfokea mtu kwasababu hajaumbwa kufokafoka. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Mkuu huyo wa nchi ameyasema hayo leo Jumamosi tarehe 2 Aprili 2022 mara baada ya kuwaapisha viongozi wateule wakiwemo mawaziri na mMwenyekiti na wajumbe wa Baraza la Maadili, Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

“Huko nyuma nilisema sitafoka, nitafanya kazi na kalamu, nitawakumbusha lakini sitafoka, hata ukinitazama sijaumbwa kuofoka foka na mimi ni mama, ni mlezi nitajaribu kuwalea lakini ulezi utakaponishinda nitachukua hatua kali.”

Amesema bado kuna kazi kuwa ya kuelemisha watumishi wa umma kuhusu dhana ya ukuaji wa kitaifa ili waondokane na dhana ya ukuaji binafsi.

“Tunapozungumza growth watu hawana picha kwamba ukuaji tunaozungumza ni wa nchi kwa ujumla, watu wanajitazama mimi kwa ujumla niko hapa nakuaje, natokaje, nakaa miaka mingapi na natoka na nini,” amesema na kuongeza:

“Hatutizami kwamba wajibu wangu nikukuza nchi, kukuza uchumi ,kuleta uimara wa taifa langu tunatizama yale madogo madogo.”

Amesema jina la Tanzania ni zuri na kama ni kuliharibu wataliharibu wote hivyo kuwataka wasaidizi wake kumsaidia kwani urais ni taasisi na si mtu.

3 Comments

  • Miradi ya kimkakati imeanza kususua. Sasa, zile “inventory” zao ziko wapi?
    Miradi isipokwisha kwa wakati tusilaumu vita ya Ukraine.
    Ripoti za madudu zimeongezeka pia. Kwa nini ubadhirifu unakua sasa.
    Mama, tembeza kalamu wakuheshimu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chongolo asikitishwa na mradi wa Mil 900 kutoanza kutoa manufaa

Spread the loveKATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu:Suluhu ya ugumu wa maisha ni Katiba Mpya

Spread the love  MAKAMU mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Bara,...

error: Content is protected !!