May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Samia kuzungumza na wazee wa Dar kesho

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Saluhu akihutubia Taifa mara baada ya kuapishwa

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kesho Ijumaa tarehe 7 Mei 2021, anatarajiwa kufanya mkutano na zaidi ya wazee 900 wa Mkoa wa Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Katika mkutano huo, Rais Samia atazungumzia masuala mbalimbali.

Leo Alhamisi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge amesema, kikao icho kitafanyika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City kuanzia saa 8 mchana.

Mkuu huyo wa mkoa ametoa wito kwa wazee waliopata mialiko ya kushiriki kikao hicho, kujitokeza kwa wingi ili wapate kusikiliza kile ambacho Rais Samia amewaitia.

error: Content is protected !!