September 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Samia kuzindua mbio za Mwenge

Spread the love

SAMIA Suhulu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mbio za Mwenge unazotarajiwa kuzinduliwa tarehe 18 Aprili mwaka huu katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro, anaandika Christina Haule.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari mjini Morogoro leo, Dk. Stephen Kebwe, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro amesema kuwa, maandalizi ya sherehe hizo yamekamilika.

Dk. Kebwe amewaagiza wakuu wa wilaya, wakurugenzi, watendaji wa Halmashauri za Wilaya, miji midogo na manispaa kusimamia kikamilifu maandalizi ya mbio hizo huku akiwahamasisha wadau mbalimbali kutoa michango yao kwa ajili ya kufanikisha tukio hilo.

Amesema, kauli mbiu ya mwaka huu inasema “Vijana ni nguvu kazi ya Taifa, washirikishwe na wawezeshwe.”

Hata hivyo amewaomba wananchi wajitokeze kwa wingi na kushirikiki kamilifu katika tukio la uwashaji Mwenge huo wa Uhuru.

error: Content is protected !!