August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Samia azindua mradi wa maji wa Sh. bilioni 2.8

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassana amezindua mradi wa maji wenye thamani ya Sh. 2.8 bilioni uliopo katika Kata ya Makongolosi wilayani Chunya mkoani Mbeya.

Mradi huo unatarajiwa kuzalisha maji lita milioni 1.5 huku eneo la mji huo wa Makongolosi likiwa na mahitaji ya maji lita milioni 1.2. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).

Uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 6 Agosti, 2022 katika siku ya pili ya ziara ya Rais Samia ambaye anaendelea kuifanya mkoani Mbeya.

Amesema yeye kama mama anatambua tatizo la wanawake wenzake ambalo ni kwenda kutafuta maji.

“Nitahakikisha nawapatia maji wananchi… leo nimekuja kutimiza ahadi hii. Ndani ya mkoa wa Mbeya kuna miradi 50, ikifika 2025 mkoa wa Mbeya tunataka upate maji asilimia 95.

“Kwa sasa mji huu unamahitaji ya lita milioni 1.2 lakini mradi huu unatoa milioni 1.5 kwa hiyo ukimalizika vijiji vyote Makongolosi watapata maji asilimia 100,” amesema.

Aidha, ametoa wito kwa watumishi watakaokuwa wanahudumia mradi huo, kuhakikisha unatoa maji siku zote kwa sababu kumekuwa na hulka ya maji kutoka wakati Rais anakwenda kuzindua, lakini akiondoka na maji yanakatika.

Awali Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Anthony Sanga amesema awali upatikanai wa maji katika mji huo ulikuwa asilimia 10 kupitia kisima kilichokuwa kimechimbwa na Shiriki la Maendeleo la Kimataifa la Denmark (Danida).

“Sasa wanapata maji asilimia 70, jumla ya vituo 20 vimejengwa ambapo wateja 585 wameunganishiwa huduma ya maji. Kuna vijiji viwili havijaunganishwa maji ambavyo ni Ujerumani na Mwaoga lakini kazi ya kuunganisha inafanyika,” amesema.

error: Content is protected !!