Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Samia aungana na viongozi Afrika kumpongeza Ruto
Habari za SiasaTangulizi

Samia aungana na viongozi Afrika kumpongeza Ruto

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan ameungana na viongozi wengine wa Bara la Afrika kwa kumpongea mshindi wa nafasi ya urais pamoja na kuwapongeza wananchi wa Taifa hilo la Afrika Mashariki kwa kufanikisha uchaguzi wa amani, haki na uwazi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Pongei hizo zimekuja wakati Kenya ikwa mbioni kupata serikali mpya baada ya jana tarehe 15 Agosti, 2022 Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya, Wafula Chebukati kumtangaza William Ruto kuwa rais mteule jana Jumatatu jioni.

Chebukati alimtangaza kiongozi huyo wa Kenya Kwanza mwenye umri wa miaka 55 kama rais mteule baada ya kuzoa kura 7,176,141 kura za mwisho. Hii ilitafsiri hadi 50.49% ya jumla ya kura halali zilizopigwa.

Kufuatia ushindi huo wa kinyang’anyiro cha Agosti 9, baadhi ya viongozi wa mataifa mbalimbali ya Afrika wamejitokeza kumpongeza naibu rais kwa kupanda ngazi na kunyakua kiti cha juu zaidi nchini.

Katika salamu zake za pongezi, Rais wa Tanzania Samia Suluhu ameandika hivi kwenye akaunti yake ya Twitter, “Ninapenda kuwapongeza kwa dhati wananchi wa Kenya kwa kushiriki uchaguzi wao mkuu kwa amani na utulivu, ambapo matokeo yake ni Dkt @WilliamsRuto kutangazwa kuwa Rais mteule wa Kenya. Tanzania itaendeleza undugu na ushirikiano wa Kihistoria na Kenya uliodumu miaka na miaka”.

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa alisema kwamba anatazamia kufanya kazi pamoja na rais mteule.

“Natoa pongezi zangu za dhati kwa Rais Mteule @WilliamSRuto wa Jamhuri ya Kenya. Kenya yenye ustawi na umoja ni sharti muhimu na mchangiaji katika bara lenye ustawi na amani. Tunatazamia kufanya kazi nawe katika kutafuta Afrika tunayoitaka.”

Rais wa Burundi, Jenerali Évariste Ndayishimiye aliwapongeza Wakenya kwa kudumisha amani wakati wa uchaguzi na kuviomba vyama vya kisiasa kupatana licha ya matokeo ya kura.

“Pongezi zangu za dhati kwa Rais Mteule WilliamsRuto na watu wa Jamhuri ya Kenya kwa kufanya uchaguzi huru, wa haki na wa amani. Tunawahimiza wahusika wote kulinda amani, na mizozo isuluhishwe kwa njia za kisheria zilizopo. Idumu jumuiya yetu.”

Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa pia alimpongeza Ruto na kuonyesha imani kuwa rais mteule atakuwa kiongozi anayeheshimika.

“Hongera William Ruto kwa kuchaguliwa kwake kama Rais ajaye wa Kenya,” aliandika kwenye Twitter.

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed kwa upande wake alimtakia rais mteule heri katika majukumu yake mapya.

“Pongezi zangu kwa William Ruto, kwa kuchaguliwa kwako kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya. Nakutakia mafanikio mema katika juhudi zako,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia atua Uturuki kwa ziara ya siku 5

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano amewasili nchini Uturuki kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

error: Content is protected !!