
RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema, ataunda kamati maalum ya kufanyia utafiti ugonjwa wa maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19) kwani “Tanzania siyo kisiwa.” Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).
Samia ametoa msimamo huo leo Jumanne, tarehe 6 Aprili 2021, katika hotuba yake baada ya kumaliza kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni wakiwemo Makati wakuu, naibu wao na wakuu wa taasisi kadhaa.
Akigusia suala la corona, Rais Magufuli amesema “nakusudia kuunda kamati ya wataalamu, waliangalie suala la COVID kitaalamu zaidi na kwa ukubwa wake halafu watushauri. Hatufai kulikataa au kulikubali pasina kulifanyia utafiti.”
“Hatuwezi kujitenga kama kisiwa na hatuwezi kupokea kila tunachoambiwa bila kufanya ya kwetu. Rais Kikwete alituambia ya kuambiwa…,” amehoji Rais Samia huku akijibiwa “changanya na yako.”
Msimamo alioutoa Rais Samia, ni tofauti na ule wa serikali iliyopita ambayo ilishindwa kuweka msimamo wake kuhusu corona na ilizuia utoaji wa taarifa na takwimu zozote kuhusu ugonjwa huo.
Pia, haikutumia njia za kisayansi kukabiliana na ugonjwa huo hatari na badala yake, ilihimiza matumizi ya njia za tiba za asili hasa za kujifukiza “kupiga nyungu” na maombi yaliyofanywa na viongozi wa dini.
More Stories
Takukuru yamkamata kigogo bandari akiwa mafichoni
Barabara Kibena – Lupembe yatengewa Bil 5.96
Tamisemi: Hospitali Biharamulo ilitengewa Mil 500