August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Samia ateua makatibu tawala wa mikoa wapya, saba watemwa

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan leo tarehe 28 Julai, 2022 amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa wapya saba na kuwahamisha vituo vya kazi 10, na wengine tisa kubaki katika vituo vyao vya kazi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus, Makatibu Tawala wapya walioteuliwa ni

 1. Kamishna Dk Mussa Ali Mussa, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro.
 2. Prof. Godius Walter Kahyarara, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita. Alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara.
 3. Mhandisi Leonard Robert Masanja, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Iringa. Alikuwa Mkufunzi wa Chuo cha Tanesco mkoani Dar es Salaam.
 4. Toba Alnason Nguvila, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kagera. Alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Mkoani Kagera.
 5. Elikana Mayuganya Balandya, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza. Alikuwa Kamishna wa Bajeti Wizara ya Fedha na Mipango.
 6. Prof. Sin Donald Tumbo, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga. Alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo.
 7. Dk John Rogath Mboya, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Tabora. Alikuwa Kamishina wa Idara ya Bajeti katika Wizara ya Fedha na Mipango.

Waliohamishwa vituo vya kazi ni pamoja na;

 1. Missaile Albano Musa, amehamishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Arusha. Alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Songwe.
 2. Rehema Self Madenge, amehamishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam. Alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Lindi.
 3. Hassan Abbas Rugwa, amehamishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Katavi. Alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam.
 4. Ngusa Dismas Samike, amehamishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Lindi. Alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza.
 5. Msalika Robert Makungu, amehamishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Mara. Alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Tabora.
 6. Msovera Albert Gabriel, amehamishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma. Alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Mara.
 7. Rodrick Lazaro Mpogolo, amehamishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya. Alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Katavi.
 8. Zuwena Omari Jiri, amehamishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Pwani. Alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga.
 9. Happiness William Seneda, amehamishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Songwe. Alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Iringa.
 10. Rashid Kassim Mchata, amehamishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa. Alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma.

Aidha, wanaoendelea katika vituo vyao vya kazi ni;

 1. Dk. Fatuma Ramadhan Mganga, anaendelea kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma
 2. Karolina Albert Mthapula, anaendelea kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Manyara.
 3. Abdallah Mohamed Malela, anaendelea kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara.
 4. Judica Haikale Omary, anaendelea kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Njombe.
 5. Willy Lugaliyulula Machumu, anaendelea kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro.
 6. Steven Mashauri Ndaki, anaendelea kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma.
 7. Dorothy Aidan Mwaluko, anaendelea kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Singida.
 8. Prisca Joseph Kayombo, anaendelea kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu.
 9. Pili Hassan Mnyema, anaendelea kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Tanga.
error: Content is protected !!