Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Samia ateta na Rais mstaafu Obasanjo Ikulu Dodoma
Habari za SiasaTangulizi

Samia ateta na Rais mstaafu Obasanjo Ikulu Dodoma

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Nigeria, Olusegun Obasanjo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Mazungumzo hayo, yamefanyika leo Jumatatu, tarehe 3 Mei 2021, Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma.

Obasanjo ametoa salamu zake za rambirambi kwa Rais Samia, kufuatia vifo vya waliokuwa marais wa wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa na Hayati John Pombe Magufuli.

Hayati Mkapa, alifariki dunia tarehe 23 Julai, 2020 na Hayati Magufuli, aliaga dunia tarehe 17 Machi, 2021.

Rais huyo mstaafu, amempongeza, Rais Samia kwa kupokea kijiti cha kuwa Rais wa Tanzania na amemtakia heri katika majukumu yake.

Aidha, katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamezungumzia hali ya usalama Barani Afrika na umuhimu wa wakuu wa nchi kujadiliana na kutafuta suluhisho la migogoro hiyo ambayo inasababisha vifo vya watu wasio na hatia hasa wanawake na watoto.

Pia, viongozi hao, wamezungumzia masuala ya maendeleo hasa katika uchumi na kusisitiza umuhimu wa nchi za Afrika kuongeza ushirikiano na kuondoa vikwazo vya biashara na uwekezaji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!