Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Samia ataka utaratibu wa usuluhishi upewe kipaumbele
Habari za Siasa

Samia ataka utaratibu wa usuluhishi upewe kipaumbele

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema ni vyema utaratibu wa usuluhushi upewe kipaumbele katika utatuzi wa migogoro mbalimbali kutokana na faida zake ikiwemo kupunguza gharama na kufupisha muda wa mashauri na upatikana haki. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Mkuu huyo wa nchi ametoa wito huo leo Jumatano tarehe 1 Februari, 2023 katika madhimisho ya kilele cha siku ya Sheria nchini ambapo ameoneshwa kufurahishwa na kauli mbiu yake inayosema ‘Umuhimu wa Utatuzi wa Migogoro kwa Njia ya Usuluhishi Katika Kukuza Uchumi Endelevu: Wajibu wa Mahakama na Wadau’.

Rais Samia amesema sheria mbalimbali zimetoa nafasi ya ushuluhishi kwa kuweka mabaraza mbalimbali ya usuluhishi.

Hata hivyo amesisitiza muhimu wa kutoa mafunzo yanayolenga usuluhishi wa migogoro kwa mabaraza ya usuluhishi kwani hivi sasa hayafanyi hivyo.

“Ifike mahala Watanzania waone kwamba kufikishana mahakamani sio jambo la lazima ila tu pale inapobidi na badala yake usuluhishi iwe ndiyo njia ya kwanza ya kukimbiliwa,” amesema Rais Samia

Rais Ssmia ameonesha kufurahishwa na mafanikio yaliyopatikana kupitia kituo cha usuluhishi tangu kianzishwe mwaka 2015 ambapo kati ya mashauri 354 yaliyosajiliwa katika kituo hicho mwaka jana 2022 peke yake kituo kimesuluhisha kwa ukamilifu mashauri 64 huku mengine saba yakiwa kwenye hatua nzuri za kufikia muafaka.

“Na kazi hii ikiendelea tutakuwa na uhakika kwamba haki itapatikana kwa haraka kupia usuluhishi na inaonekana sasa watu wameanza kuona faida za suluhishi na hivyo tuzidi kuhakikisha kuwa kasi ya mashauri yanaisha kupitia usuluhishi inaongezeka.

Amesema hana shaka na suala la uboreshaji wa kanuni za usuluhishi kwani suala hilo ni endelevu kulingana na mahitaji ya kipindi husika.

“Kama alivyosema Jaaji Mkuu kwamba kanuni hizi zitakwenda na kubadlika kuendana na aina ya kesi jinsi mtakavyokuwa manazipokea na kuzipanga katika mafungu yake,” amesema.

Ameitaka mahakama kuendelea kadri ya uhitaji lakini pia amesisitiza umuhimu wa utafiti ili zipatikane njia mbadala za usuluhishi.

Hata hivyo amesisitiza umuhimu wa imani ya mteja kwa wasuluhishi, “Wale wasuluhishi wanajenga imani gani kwa wateja hilo nalo ni jambo kubwa kwasababu katika vituo vyetu hivi vya ndani au international wawekezaji wanapokuja na kusililizwa wanataka kupewa imani na imani haitapatikana mpaka waone kesi moja mbili zimetolewa maamuzi mema ambayo yamewaridhisha wao yamewaridhisha walioshtakiana nao,”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!