Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Samia apitishwa 100% kugombea uenyekiti CCM
Habari za SiasaTangulizi

Samia apitishwa 100% kugombea uenyekiti CCM

Spread the love

 

HALMASHAURI Kuu ya chama tawala- Chama Cha Mapinduzi (CCM), nchini Tanzania, imempitisha kwa asilimia 100, mjumbe wa kamati kuu ambaye ni Rais, Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea pekee wa nafasi ya uenyekiti chama hicho. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Rais Samia, amepitishwa leo Alhamisi, tarehe 29 Aprili 2021, katika kikao cha halmashauri kuu, kilichokutana, katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Convetion Center, jijini Dodoma, chini ya Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula.

Ni maandalizi ya mkutano mkuu maalum, utakaofanyika kesho Ijumaa, jijini humo, ukiwa na agenda kuu moja ya kumthibitisha Rais Samia kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Hayati Rais John Pombe Magufuli.

Hayati Magufuli, alifikwa na mauti akiwa madarakani, tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena, Makumbusho mkoani Dar es Salaam. Mwili wake, ulizikwa nyumbani kwao, Chato mkoani Geita.

Katibu wa Itikadi na Uenezi , Humphrey Polepole akizungumza na vyombo vya habari baada ya kumalizika kwa kikao cha halmashauri kuu, amesem mgombea wa nafasi ya mwenyekiti atakuwa mmoja.

Amesema kikao hicho, kimepitisha azimio la kupeleka jina moja la Samia Suluhu Hasani kwenye mkutano mkuu maalum ambao utapiga kura ya kumchagua mwenyekiti.

Polepole amesema, katika mkutano huo, wajumbe takribani 1,876 watashiriki wakiwemo viongozi wote wa vyama vya siasa vilivyosajiliwa, vyama rafiki kutoka nje ya nchi.

Pia, amesema, halmashauri kuu, imewapitisha wajumbe watatu ambao watasimamia uchaguzi huo ambao ni; Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai; Zuberi Maulid, mjumbe kutoka Baraza la wawalishi pamoja na Gaundensia Kabaka, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT).

Aidha amesema, mkutano huo ,hakutakuwa na burudani wala shangwe na nderemo kama ilivyo desturi kunapofanyika mkutano kuu kutokana na chama bado kipo kwenye majonzi ya kumpoteza Hayati Magufuli na badala yake, kutaimbwa nyimbo mbili kutoka bendi ya chama hicho.

Polepole ambaye pia ni mbunge wa kuteuliwa, amesema kwa kauli moja, halmashauri kuu ina imani kubwa kwa Samia Suluhu Hassan kutokana na uaminifu, uzalendo, uadilifu na mapenzi mema juu ya chama.

“Tuna imani na Rais Samia Suluhu Hassan kwani amekuwa mjumbe wa kamati kuu, amekuwa mlinzi wa amani, mlezi wa demokrasia na mpenda watu hivyo tunaimani ni mtu sahihi anayeweza kuvaa viatu vya Hayati Dk. John Magufuli, ndiyo maana azimio limeungwa na wajumbe wote,” amesema Polepole.

Katika hatua nyingine, halmashauri kuu ya CCM, imefanya uteuzi wa majina ya wanachama 700 ambao waliomba kuteuliwa katika nafasi mbalimbali zilizo wazi, kuanzia ngazi ya wilaya mpaka Taifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!