Monday , 5 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Samia aomba ripoti fedha zilizotolewa hazina Januari-Machi
Habari MchanganyikoTangulizi

Samia aomba ripoti fedha zilizotolewa hazina Januari-Machi

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemuagiza Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Prof. Florence Luoga na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere, wampatie ripoti ya matumizi ya fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo, zilizotolewa hazina kuanzia Januari hadi Machi 2021. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Agizo hilo la Rais Samia limetolewa leo tarehe 28 Machi 2021, siku tisa tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Tanzania, akirithi mikoba ya Dk. John Magufuli, aliyefariki dunia tarehe 17 Machi mwaka huu, katika Hospitali ya Mzena, Makumbusho mkoani Dar es Salaam.

Akizungumza Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, Rais Samia amewaagiza viongozi hao kumpatia ripoti hiyo, ili aone namna zilivyotumika.

“….CAG, naomba nenda pitia na gavana wa benki kuu yuko hapa, fedha zote zilizotolewa Januari hadi Machi zilizoenda katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo nataka kuziona,” ameagiza Rais Samia.

Rais Samia ametoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020, iliyobainisha ubadhirifu katika mashirika ya umma.

“Kwa upande wake CAG niwashukuru sana kwa ripoti yenu ya kina, ambalo ningependa kujielekeza nalo, la kwanza mahshirika ya umma hayana hati mbaya lakini upotevu unatokea huko, na uliniambia hali si shwari. Naomba nitoe agizo kwako na Takukuru na CAG mfanyie kazi suala hilo,” ameagiza Rais Samia.

Rais Samia ametoa agizo hilo kwa CAG Kichere na Prof. Luoga, kwa mara ya kwanza, tangu aapishwe tarehe 19 Machi 2021, kuwa Rais wa Awamu ya Sita wa Tanzania.
Mwanamama huyo ameapishwa kuwa Rais wa Tanzania kufuatia kifo cha Dk. Magufuli, aliyefariki dunia akiwa madarakani, miezi minne tangu alipoapishwa kuendelea na muhula wake wa mwisho wa Serikali ya Awamu ya Tano.


Dk. Magufuli aliapishwa kuongoza tena Tanzania tarehe 5 Novemba 2020, baada ya kushinda kiti cha urais katika Uchaguzi Mkuu, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kwa mara ya kwanza Dk. Magufuli aliingia madarakani tarehe 5 Novemba 2015, baada ya kushinda uchaguzi mkuu.

Mwanasiasa huyo aliiongoza Tanzania katika kipindi cha miaka mitano na miezi mitano mfululizo (Novemba 2015-Machi 2021), hadi umauti ulipomfika, huku Mama Samia akiwa makamu wake wa rais.

Dk. Magufuli alifariki dunia kwa matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo, na mwili wake ulizikwa Ijumaa tarehe 26 Machi 2021, kijijini kwao Chato mkoani Geita.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tunduma watenga 60 milioni kujenga machinjio ya kisasa

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma Imetenga kiasi cha Tshs Miloni 60...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 17 kujenga bandari kavu Tunduma

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma iliyopo wilayani  Momba mkoani Songwe imepatiwa...

Habari Mchanganyiko

Bandari ya Kigoma kuongezewa uwezo wa kutoa huduma zake

Spread the love  SERIKALI kupitia mamlaka ya Bandari nchini (TPA), imewekeza takribani...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kifo cha mwanafunzi UDOM: Tume yamsafisha naibu waziri

Spread the loveTUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini (THBUB),...

error: Content is protected !!