November 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Samia akemea ‘vita’ ya uwekezaji

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amekemea vita baina ya wawekezaji hasa wanaozalisha bidhaa zinazofanana. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza kabla ya kuzindua maonesho ya bidhaa zinazozalishwa na viwanda vilivyomo Mkoa wa Pwani leo tarehe 29 Oktoba 2018, Samia amesema, hakuna haja ya wawekezaji kupigana vita wenyewe kwa wenyewe bali watafute njia ya kuboresha bidhaa zao ili zipate soko.

Samia amesema, katika Mkoa wa Pwani kuna changamoto ya wawekezaji kupigana vita, ambapo ameutaka uongozi wa mkoa huo kukaa na wawekezaji ili kuondoa changamoto hiyo.

“Changamoto ni kupigana vita wawekezaji kwa wawekezaji, hasa wa bidhaa zinazofanana, uongozi wa mkoa uangalie hilo, hakuna haja wawekezaji kwa wawekezaji kupigana vita, mkuu wa mkoa hilo nakuachia wewe kwa sababu unajua uwekezaji wako,” amesema.

Katika hatua nyingine, Samia amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Everist Ndikilo kuingia makubaliano na wawekezaji wanaotumia malighafi zinazochimbwa, ili wapande miti katika mashino wanayochimba, kuepuka maeneo kuwa jangwa.

error: Content is protected !!