Katika ujumbe wake, kupitia ukurasa wake wa twitter, Rais Samia amesema, klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, imeandika historia na imelipa hadhi kubwa taifa lake.
“Hongereni sana Yanga kwa hitimisho la mchezo wa fainali. Historia mliyoandika katika safari yenu ya michuano hii ni kubwa na ya heshima kwa taifa letu. Nawatakia kheri katika mipango yenu katika siku zijazo,” ameeleza.
Yanga iliyokuwa inashiriki michuano hiyo, imekuwa timu ya kwanza katika kipindi cha miongo mitatu iliyopita, kufika fainali ya michuano ya CAF.
Katika mchezo wake wa jana wa fainali dhidi ya USM Alger, klabu hiyo ya mitaa ya Twiga na Jangwani, ilishinda kwa goli moja lililofungwa kwa njia ya penati na Djuma Shaban.
Hongereni sana Yanga kwa hitimisho la mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup). Historia mliyoandika katika safari yenu ya michuano hii ni kubwa na ya heshima kwa Taifa letu. Nawatakia kheri katika mipango yenu ya siku zijazo. pic.twitter.com/m0s1Q0qslg
— Samia Suluhu (@SuluhuSamia) June 4, 2023
Ndoto za Yanga kutwaa Kombe la Shirikisho zimefifishwa na mabao ya ugenini licha ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika fainali ya pili dhidi ya USM Alger.
Yanga waliandika historia yao mpya tangu kuanzishwa kwake mwaka 1935 kufikia hatua hiyo na kwa kushinda ugenini, katika mechi ya marudiano ya fainali ya kombe hilo.
Yanga imekosa taji la kwanza la CAF kutokana na faida ya bao la ugenini kuwabeba Waalgeria.
Wenyeji ilitwaa taji hilo la kwanza kwao baada ya awali kushinda ugenini 2-1 na matokeo ya jumla kuwa sare ya 2-2, lakini kanuni ya bao la ugenini ikawapata taji hilo kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa 5 Jullieti 1962 mjini Algers.
Yanga walionyesha kiwango kikubwa cha mchezo ugenini tofauti na ilivyocheza jijini Dar.
Kocha Nasreddine Nabi aliwatumia mabeki watano, ikiwamo Dickson Job kama kiungo namba sita na kuwabana wenyeji na kufanikiwa kupata bao hilo pekee dakika ya saba tu likiwekwa kimiyani kwa penalti na beki Djuma Shaban baada ya Kennedy Musonda kuchezwa madhambi.
Kanuni za CAF zinaeleza, pale matokeo yanapolingana, huangalia timu ipi iliyoshinda magoli mengj ugenini; kanuni ambayo imedumu kwa miaka mingi sana duniani.
Hata hivyo, katika siku za karibuni, hasa kwenye michuano ya UEFA, kanuni hii imefutwa na hivyo, kama ingekuwa UEFA, mechi ya jana ingeongezwa dakika 30 au ingekwenda penalti moja kwa moja.
Spread the love NAJUA umesikia na unazijua Derby nyingi kutoka jiji la London,...
By Mwandishi WetuSeptember 24, 2023Spread the love USHINDI huu ni wako mteja wa Meridianbet kama mechi...
By Mwandishi WetuSeptember 22, 2023Spread the love ANITWA Pablo Martín Páez Gavira ‘Gavi’, sasa ni mchezaji...
By Mwandishi WetuSeptember 21, 2023Spread the love KAMPUNI ya Bia ya Serengeti Breweries Ltd (SBL) kupitia...
By Mwandishi WetuSeptember 20, 2023
Leave a comment