November 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Samia afanyia mabadiliko Baraza la Mawaziri

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan, amefanyia mabadiliko madogo, baraza lake la mawaziri. Katika mabadiliko hayo, mwanadiplomasia mashuhuri nchini, Balozi Liberata Mulamula, ameachwa kwenye baraza hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …(endelea).

Balozi Malamula, alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Nafasi yake, imechukuliwa na Dk. Stergomena Lawrance, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Naye Inocent Bashungwa, aliyekuwa wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), amefanywa kuwa waziri wa Ulinzi.

Kwa upande wa Tamisemi, Rais Samia amempa wadhifa wa uwaziri, Angellah Kairuki; ili kukidhi takwa hilo la kikatiba, rais amemteuwa mwanasiasa huyo ambaye aliwahi kuhudumu katika utawala wa awamu ya kwanza wa Rais John Magufuli na Jakaya Kikwete, kuwa mbunge wa Bunge la Muungano.

error: Content is protected !!