January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Samatta nahodha mpya wa Taifa Stars

Spread the love

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa, amemtangaza mshambuliaji Mbwana Ally Samatta kuwa nahodha mpya wa timu hiyo, akichukua nafasi ya Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’.

Mkwasa amesema uamuzi huo umetokana na kazi nzuri ya Samatta kuitangaza Tanzania na Taifa Stars kimataifa.

Mkwasa amesema, Samatta anastahli kuwa Nahodha wa timu ya Taifa ingawa wamekuwa na Nahodha ambaye anastahili kuendelea, lakini wameona kitu pekee cha kumlipa Samatta kwa sasa ni beji ya unahodha.

Mkwasa amesema kuanzia sasa Cannavaro atakuwa nahodha wa kikosi cha wachezaji wanaocheza nyumbani kwa ajili ya michuano ya CHAN, wakati John Bocco atakuwa nahodha msaidizi wa Taifa Stars chini ya Samatta.

error: Content is protected !!