Tuesday , 3 October 2023
Home Gazeti Tangulizi Samatta, Edo kumwembe, Mobetto watoa neno, mara baada ya kuteuliwa kuwa mabalozi
Tangulizi

Samatta, Edo kumwembe, Mobetto watoa neno, mara baada ya kuteuliwa kuwa mabalozi

Mbwana Samatta
Spread the love

MARA baada ya kuteuliwa kuwa mabalozi wa kuamasisha ulipaji kodi na Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba, mwanandika Mbwana Samatta, mchambuzi wa soka Edo Kumwembe pamoja na mwanamitindo Hamisa Mobetto wametoa neno mara baada ya uteuzi huo leo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mwigulu amefanya uteuzi huo jana Bungeni, jijini Dodoma wakati akijibu hoja za wabunge wakati wa kupitishwa kwa bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Kupitia ukurasa zao kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, kwa nyakati tofauti mabalozi hao waliandika maneno ya shukrani kwa nafasi hiyo.

Mwandinga mchezaji Mbwana Samataa ambaye pia ni Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ anyekipiga kwenye klabu ya Fenerbahce ya Uturuki nakuahidi kushirikiana na mamlaka husika katika zoezi hilo.

“Kwa moyo mkunjufu Nimepokea kwa furaha ubalozi huu wa kuhamasisha walipa kodi kwa hiyari Na Nnaahidi kushirikiana bega kwa bega na mamlaka husika katika kuhamasisha Na kuelezea faida za ulipaji kodi kwa nchi yetu.”

“Naamini watanzania ni watu waelewa na haitatumika nguvu kubwa katika kuwaelewesha Na wakaelewa.”Alaindika Samatta

Edo kumwembe, mchambuzi wa Soka

Kwa upande wa Edo Kumwembe ambaye ni mchambuzi wa soka kutoka kituo cha Radio cha Wasafi Fm, aliandika kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kuwa, atafanya kazi hiyo kwa kuangalia maslai ya nchi mbele.

“Asante Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu nchemba, kuamini kwamba mimi naweza kuwa balozi wa uhamasishaji wa kulipa kodi kwa hiyari kwa watanzania na wageni wanaokuja nchini.”

“Nitaifanya kazi hii kwa maslahi mapana ya taifa nikishirikiana na mabalozi wengine uliowateua.” Aliandika Edo Kumwembe

Hamisa Mobetto, mwanamitindo

Nae mlimbwende Hamisa Mobetto hakuwa nyuma yeye alisema kuwa anashukuru serikali kwa kuendelea kuamini vijana kwenye ujenzi wa Taifa.

“Ni heshima kubwa sana kuteuliwa kuitumikia nchi yangu. Ni heshima kubwa kuliko maneno ninayoweza kutumia kuielezea!”

“Nimshukuru Pia Rais wangu Mama Samia Suluhu Hassan na serikali nzima akiwemo Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba kwa kuendelea kuamini vijana kwenye ujenzi wa Taifa letu!” Alisema Mobetto

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kupokea ndege ya 14 ya ATCL, safari kuongezeka

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania, kesho tarehe 3 Oktoba 2023, inatarajia...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mobhare Matinyi Msemaji mpya wa Serikali

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa Mkuu wa...

Habari MchanganyikoTangulizi

Basi la Magereza lagonga treni yenye abiria 650 Dar

Spread the loveBasi  Jeshi la Magereza lenye namba MT 0040 limegonga treni...

Habari MchanganyikoTangulizi

Afya ya akili yatajwa chanzo kuvunjika ndoa

Spread the loveCHANGAMOTO ya afya ya akili, imetajwa kuwa chanzo cha migogoro...

error: Content is protected !!