October 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Samatta dimbani leo dhidi ya Arsenal

Mbwana Samatta

Spread the love

NAHODHA wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Ally Samatta leo atashuka tena dimbani kwenye Ligi Kuu nchini England ambapo klabu yake ya Astorn Villa itakapo ikaribisha Arsenal kwenye uwanja wa Villa Park. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Astorn Villa ambayo ina pointi 31 na kushika nafasi ya 18 kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza michezo 36 na kuwa kwenye hatari ya kushuka daraja.

Mchezo huo ambao utakuwa muhimu kwa kila timu kutokana na Arsenal kuhitaji matokeo ili  kujiweka vizuri kuelekea mchezo wa fainali wa kombe la FA dhidi ya Chelsea baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Manchester city kwenye mchezo wa nusu fainali.

Samatta ambaye alijiunga na timu hiyo kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Januari, 2020 akitokea KRC Genk watakuwa na kibarua kikubwa mbele ya Arsenal ili kujinasua kushuka daraja ambapo tayari timu ya Norwich imeshashuka.

error: Content is protected !!