January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Samatta amlilia Rais Magufuli

Rais John Magufuli

Spread the love

 

NAHODHA wa timu ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Mbwana Samatta amewaomba wananchi, kushikamana katika kipindi hiki cha majonzi ya kumpoteza, Rais John Pombe Magufuli (61). Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea)

Samatta anayekipiga katika klabu ya Fenerbahçe ya Uturuki, ametoa ombi hilo leo Alhamisi tarehe 18 Machi 2021, kupitia akaunti yake ya Twitter.

Nasaha hizo, amezitoa saa chache kupita, tangu Makamu wa Rais wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, alipotangaza kifo cha Rais Magufuli, aliyefariki jana Jumatano saa 12:00 jioni, katika Hospitali ya Mzena, Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu ya moyo.

Samatta ameandika “Tutakukumbuka daima milele mzee wetu, umeumaliza mwendo tunaomba kwa mungu upumzike kwa amani.”

“R.i.p Mr president 🙏🏿🙏🏿 umetuachia simanzi na majonzi. Poleni wanafamilia wa mpendwa wetu poleni watanzania wenzangu. Tuendelee kushikamana katika kipindi hiki cha majonzi,” amesema Samatta, mchezaji wa zamani wa Aston Villa ya Uingereza.

error: Content is protected !!