August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Samatta amlilia Farid Mussa

Spread the love

MSHAMBULIAJI wa KRC Genk na nahonda wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta amekuwa katika sintofahamu juu ya Farid Mussa mchezaji wa Azam FC kwenda kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Deportivo Tenerife ya ligi daraja la pili nchini Hispania kama taarifa za awali zilivyosema.

Samatta ameandika hayo kupitia ukurasa wake unaopatikana kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, juu ya nini kinachokwamisha juu ya mchezaji huyo kwenda kucheza soka la kulipwa nchini Hispania.

“Asalam aleikum? Niliposikia Farid anakwenda Hispania kwa majaribio nilipata furaha sana kwa kuwa niliamini kwa kipaji alichonacho asingeshindwa majaribio katika klabu ile na ndivyo ilivyokuwa na furaha yangu iliongezeka baada ya kusikia Azam wamemruhusu kwenda kuanza maisha mapya ya soka Ulaya, kwanini niwe na furaha kwa sababu naamini mafanikio ya timu yetu ya taifa yatapiga hatua kwa haraka tukiwa na wachezaji wengi wanaocheza soka la kulipwa nje ya Tanzania, (imani yangu) lakini kadri siku zinavyokwenda nimekuwa simsikii Farid akiwa katika klabu yake mpya na habari zilizopo ni kuwa bado yupo Tanzania wakati kila kitu kilishakwisha nani anajibu swali hili? Tafadhali? Kuna nini nyuma ya pazia.”

Ikumbukwe Mei mwaka huu uongozi wa klabu ya Azam FC ulikaririwa ukisema Farid ataondoka nchini kuelekea nchini Hispania kujiunga na timu yake hiyo mpya Tenerife baada ya fainali ya mechi ya FA dhidi ya Yanga lakini mpaka sasa hali imeonekana kuwa ni tofauti na kilichozungumzwa.

error: Content is protected !!