January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Samata aifuata tuzo ya Afrika kesho

Spread the love

MSHAMBULIAJI wa timu ya Taifa ya Tanzania na TP Mazembe, Mbwana Samata anatarajia kwenda nchini Nigeria kesho alfajiri kuhudhuria utoaji wa Tuzo za Mchezaji Bora wa Afrika kwa wanaocheza ligi za ndani. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Samata ni mmoja kati ya nyota watatu wanaowania tuzo hiyo sambamba na Robert Kidiaba wa Congo DR na TP Mazembe na mshambuliaji wa Algeria na Etoile du Sahel, Baghdad Boundjah (Algeria).

Mshambuliaji huyo ataongozana na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine akiwa kama mwakilishi wa serikali jijini Abuja, Nigeria.

Mwesigwa anatarajiwa kuondoka na Samatta kuelekea Nigeria katika mji wa Abuja ambapo sherehe za utoaji tuzo hizo zitafayika  Alhamisi Januari 7, ambapo siku ya sherehe hizo Katibu Mkuu ataambatana na Ofisa ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria.

Mbwana Samatta anawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani, huku pia akiwa mfungaji bora wa michuano ya Ligi ya Mabingwa (CAF CL) baada ya kuifungia klabu yake ya TP Mazembe mabao nane na kuibuka mabingwa wapya wa michuano hiyo.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtakia kila la kheri Mbwana Samatta katika kinyanganyiro hicho cha uchezaji bora na kusema kwa niaba ya watanzania wote wanamuombea dua njema aweze kuibuka mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani.

error: Content is protected !!