Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Samaki wa Sh. 20 milioni wataifishwa Mwanza
Habari Mchanganyiko

Samaki wa Sh. 20 milioni wataifishwa Mwanza

Sehemu ya samaki waliovuliwa kwa uvuvi haramu
Spread the love

SERIKALI mkoani Mwanza, imekamata na kuwataifisha samaki kilogramu 3482 wenye thamani ya Sh. 20,892,000 waliovuliwa ‘kimagendo’ na wavuvi haramu kinyume na sheria za uvuvi zinazoelekeza samaki kuvuliwa kuanzia sentimita 51 hadi 84, anaandika Moses Mseti.

Samaki hao aina ya sangara waliovuliwa wilaya ya Ukerewe mkoa wa Mwanza, ni sentimita 50 (wachanga) na 85 wazazi wasioruhusiwa kuvuliwa kwa kuwa bado wanaendelea kuzaliana kwa mjibu wa sheria ya uvuvi ya mwaka 2003.

Tukio la kukamatwa kwa samaki hao, limefanywa na Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoa wa Mwanza na maafisa uvuvi wilaya ya Ilemela, baada ya taarifa za kuwepo gari yenye namba T. 202 BGE eneo la Nyehunge lililokuwa limebeba samaki hao.

John Mongella, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, amesema vitendo vya uvuvi haramu nchini vinachangiwa na baadhi ya maafisa uvuvi wasiokuwa waaminifu kwa kupokea rushwa kutoka kwa wavuvi.

Amesema kuwa kitendo cha maafisa uvuvi kushindwa kutekeleza wajibu wao, kimechangia kuendelea kuwepo kwa uvuvi haramu jambo ambalo alidai hawatavumilia kuendelea kuwepo na kupoteza raslimali za Taifa kwa uzembe wa watu wachache.

“Kama Maafisa wa Serikali, wakiwa ndio vinara wanao wasaidia wavuvi haramu ni bora tukafanye kazi nyingine, maana kama ni kazi zakufanya zipo nyingi, tutaendelea kutumia rasilimali za taifa na vita hii haitakoma kwa maafisa kuendelea kushirikiana na wavuvi haramu.

“Takukuru imekamata mhalifu alafu afisa uvuvi (Ivon Maha) awaruhusu waondoke na kibali cha kusafirishia mzigo husika, isitoshe mhusika hana leseni, kwa nini tusiseme upo kwenye payroll (malipo) ya wahalifu,” amesema Mongella.

Ivon Maha, Afisa Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, alieleza kuwa baada ya Samaki hao kukamatwa na Takukuru, wao kama watalaamu wa masuala ya samaki waliwachambua na kisha kubaini kilogramu 2,316 wenye thamani ya Shilingi 13,896,000 walikuwa wanakidhi viwango.

Amesema samaki wengine ambao ni kilogramu 3482 wenye thamani ya zaidi ya Sh. 20 milioni ndio hawakukidhi vigezo na hao ndio waliendelea kushikiliwa na serikali mpaka walipotaifishwa na watapewa makundi yasiojiweza.

Maha amesema kutokana na hali hiyo, maafisa wa Takukuru waliruhusu samaki hao wachukuliwe na mhusika, kauli ambayo ilikanushwa vikali na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mwanza, Ernest Makale mbele ya Mongella.

Maha, amesema kwa mujibu wa sheria ya uvuvi namba 22 ya mwaka 2003, kifungu cha 40 (1) na kanuni za uvuvi za mwaka 2009 kanuni ya 50 (1) mtuhumiwa akikiri kosa hulipa faini kama alivyofanya mtuhumiwa aliekamatwa na mzigo wa samaki.

Ernest Makale, Mkuu wa Takukuru mkoa wa Mwanza, alikana kuhusika na uondoshwaji wa baadhi ya samaki waliokuwa na vigezo baada ya kuchambuliwa huku akidai kwamba wao baada ya kuwakamata waliwakabidhi kwa wataalamu wa uvuvi.

Mkoa wa Mwanza upo katika mapambano ya vita dhidi ya uvuvi haramu ambapo tayari wavuvi haramu, Nyavu za makila na zana nyingine za uvuvi zimekwisha kamatwa kwenye maeneo ya Buchosa, Ilemela na Sengerema na kuteketezwa kwa Nyakati tofauti.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!