December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sam Misago, Charles, Rwenyagira wamfuata Zembwela Wasafi Radio

Spread the love

KITUO cha Radio cha Wasafi kimezidi kuibomoa East Afrika Radio baada ya kuwang’oa watangazaji wengine watatu ambao wamejiunga na radio yao hivi karibuni. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Ikiwa ni wiki mbili baada ya kituo hicho kumuondoa Mtangazaji nguli wa East Afrika TV na Radio, Hilary Daudi ‘Zembwela,’ nyota wengine , Charles William, mtangazi wa kipindi cha East Africa Breakfast, David Rwenyagira wa East Africa Drive na Sam Misago wa E News na Friday Night Live (FNL).

Charles ambaye alipotea hewani ghafla katika kipindi hicho, ameliambia MwanaHALISI Online kuwa; “Nimeachana na East Africa Radio tangu 24 Oktoba, 2019 baada ya kufanya nao kazi tangu Julai, 2018. Naushukuru uongozi wa kituo hicho na wafanyakazi wote kwa ushirikiano waliompatia.”

Charles amesema kuhusu kipindi gani atakachokua akitangaza kitawekwa hadharani mara baada ya taratibu za kiofisi zitakapokamilika.

error: Content is protected !!