March 7, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Salah mikononi kwa Polisi

Spread the love

MSHAMBULIAJI wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri, Mohammed Salah ameingia matatizoni na polisi wa Merseyside baada ya kuibuka kwa video mitandaoni akionekana kuendesha gari huku akiwa anatumia simu yake ya mkononi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Polisi jijini Liverpool wamethibitisha tukio hilo kupitia ukurasa wao unaopatikana kwenye mtandao wa twitter na kusema kwamba video hiyo imekabidhiwa kwenye kitengo husika.

Video hiyo ambayo ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha mchezaji huyo akiwa anatumia simu yake huku akiwa amesimamisha gari lake kwa muda baada ya kuzingirwa na mashabiki wakiwemo watoto, kisha akaamua kuondoa gari akiwa bado anatumia simu yake.

Hata hivyo uongozi wa klabu ya Liverpool ulitoa taarifa ya kuwa imewafahamisha polisi wa Merseyside kuhusu video hiyo baada ya kushauriana na mchezaji mwenyewe na kujua nini kilitokea wakati tukio hilo linafanyika.

error: Content is protected !!