Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Michezo Salah, Mane tishio tuzo BBC
Michezo

Salah, Mane tishio tuzo BBC

Mohamed Salah
Spread the love

BAADA ya kutoka kwa orodha ya wachezaji watakao wania tuzo za BBC ya Mchezaji wa bora wa kandanda barani Afrika mwaka 2018, nafasi kubwa imeonekana bado ipo kwa wachzaji wanakipiga katika klabu ya Liverpool, Sadio Mane na Mohammed Salah kutokana kuwa na takwimu nzuri kwenye msimu uliomalizika. Anaripoti Kelvin Mwaipungu …  (endelea).

Wachezaji hawa wote kwa pamoja walifunga jumla ya mabao 42, kwenye Ligi Kuu nchini England wakiwa na Liverpool kwenye msimu uliomalizika na huwenda ikatumika kama kigezo kwa wapiga kura kwenye utoaji wa tuzo hiyo.

Sambamba na kuifikisha timu hiyo kwenye fainali ya klabu bingwa barani Ulaya dhidi ya Real Madrid katika msimu uliomalizika huku wakiwa wachezaji wakutumainiwa, licha ya kupoteza mchezo huo kwa mabao 3-1.

Salah alifunga jumla ya mabao 32, kwenye michezo aliocheza kwenye Ligi Kuu nchini England msimu uliopita na kuibuka kinara wa ufungaji, huku Mane akifunga jumla ya mabao 10.

Takwimu hizi huenda zikawabeba wawili hao kwenye tuzo hizo ambazo zinatarajiwa kufanyika 14 Disemba, 2018 huku ikumbukwe Salah ndiyo mshindi wa tuzo hii mwaka uliopita kutokana kuwa katika kiwango bora akiwa na klabu yake pamoja na timu ya Taifa alipoifanikisha kufuzu kwa fainali za kombe la Dunia lililofanyika Juni mwaka huu.

Wachezaji wengine ambao watawania tuzo hii ni pamoja na beki wa kati wa Juventus Medhi Benatia 31, ambaye ameshinda mataji ya Ligi Kuu mara nne mfululizo katika klabu mbili tofauti, mawili kati ya hayo akiwa na Bayern Munich, huku alifanikiwa kuingoza Morocco katika fainali za kombe la Dunia mwaka huu.

Mlinzi wa Napoli Kalidou Koulibaly, 27 ambaye ni moja kati ya walinzi bora kwenye Ligi Kuu nchi Itaria, Seria A, ambaye pia aliiongoza timu ya taifa ya Senegal kwenye michuano ya kombe la Dunia nchini Urusi na kucheza dakika zaote 270.

Na mchezaji wa mwisho ni kiungo wa kati wa Atletico Madrid Thomas Partey, 25, ambaye ni mchezaji wa kikosi cha kwanza chini ya kocha Diego Simeone, na timu ya taifa ya Ghana ambaye pia alikuwa na kiwango bora kwenye michuano ya kombe la Dunia iliyofanyika Juni Mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Meridianbet yaibukia Tandika, yafungua duka jipya

Spread the love BAADA ya kupita maeneo mbalimbali hatimae kampuni yaMeridianbet imeibukia...

BiasharaMichezo

Ukiwa na Meridianbet ni rahisi kuwa milionea

Spread the love  CARABAO Cup raundi ya 3 Uingereza inaendelea na mechi...

Michezo

Jezi ya Samatta iliyoifunga Liverpool kuuzwa Genk

Spread the love  KLABU ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji imeamua kuanza...

BiasharaMichezo

Hii ndio historia ya El-Clasico, derby bora zaidi duniani

Spread the love  KILA nchi ina vilabu viwili hasimu na pinzani nje...

error: Content is protected !!