MTENDAJI Mkuu wa klabu ya Simba, Barbara Gonzalez amemaliza sintofahamu juu ya winga wa timu hiyo, Bernard Morrison kuhusu taarifa zilikuwa zinaeleza kuwa anatakaiwa kufanyiwa upasuaji enia na kudai mchezaji huyo ni mzima wa afya na hana tatizo lolote. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).
Siku za hivi karibuni kulizagaa taarifa ya kuwa mchezaji huyo anahitajika kufanyiwa upasuaji mara baada ya kutoonekana uwanjani na klabu yake hiyo kwa muda mrefu bila sababu yoyote kutoka kwenye uongozi wa Simba.
Uvumi huo ulizidi kuenea mabpo mchezaji huyo alisafiri na timu visiwani Zanzibar kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi lakini hakucheza mchezo hata mmoja katika michezo minne Simba waliocheza visiwani humo.

Akijibu swali kwa waandishi wa Habri juu ya ukweli wa taarifa hizo, Barbara alisema mchezaji huyo alikuwa anaumwa kwenye mwezi Desemba 2020 ndio maana hakuonekna uwanjani muda mrefu ila kwa sasa yupo sawa na hivi karibuni ataingia kambini na wenzake kwa ajili ya maandalizi ya kombe la Simba Super Cup.
“Bernard Morrison yupo fiti na hana tatizo lolote bali alikuwa anaumwa kidogo mwezi Desemba mwaka jana ila kwasasa ni mzima kabisa na anafanya mazoezi kama kawaida na siku ya jumapili ataingia kambini na wenzake,” alisema Barbara.
Licha mtendaji huyo kueleza kuwa mchezaji huyo alikaa nje ya uwanja kutokana na kuumwa lakini taarifa za ndani zinaeleza kuwa Simba hawakumtumia mchezaji katika michezo mbalimbali kutokana na kuzuiliwa na mahakama na usuluhishi wa kimichezo (CAS) mara baada ya klabu ya Yanga kukata rufaa kwenye mahakama hiyo kuhusu kesi yao ya kimakataba na mchezaji huyo.
Morrison alijiunga na Simba akitokea Yanga tarehe 8 Agosti 2020 licha ya Yanga kusema bado wanamkataba naye wa miaka miwili lakini baadae akashinda kesi hiyo kupitia kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji ikabaliki iliyokuwa chini ya Mwenyekiti, Wakili Elias Mwanjala.
Leave a comment