Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Sakata mahindi yenye sumu lawaibua TPSF
Habari Mchanganyiko

Sakata mahindi yenye sumu lawaibua TPSF

Spread the love

 

SAKATA la kuzuiwa kwa mahindi yaliyodaiwa kuwa na sumu kuvu, katika mpaka wa Namanga mkoani Arusha, unaounganisha nchi ya Kenya na Tanzania, limeifanya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kuitisha kongamano, anaripoti Jemima Samwel, DMC… (endelea).

Kongamano hilo limefanyika leo Ijumaa, tarehe 28 Mei 2021, katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha wadau wa sekta ya kilimo, wakiwemo wakulima, wasafirishaji na wataalamu, kwa lengo la kujadili suala la sumu kuvu.  Ili kukuza uelewa kwa wakulima na wafanyabiashara.

Sakata hilo liliibuka mwanzoni mwa 2021, baada ya Serikali ya Kenya kuzuia  mahindi hayo yasiingizwe nchini humo, ikidai yalikuwa na kiwango cha juu cha sumu kuvu, na kwamba kama yangeingizwa yangeathiri afya za raia wake.

Akizungumzia kongamano hilo, Francis Nanai, Mkurugenzi wa TPSF amesema, litaongeza uelewa mpana juu ya sumu kuvu.

“TPSF tuliona umuhimu wa kufanya kongamano hili na ni kwa sababu ya umuhimu wa zao la mahindi, kama zao la chakula na zao la biasahara,” amesema Nanai.

Nanai amesema “hivi karibuni kulikuwa na sintofahamu kati ya Tanzania na Kenya mpakani kwa sababu ya tatizo la sumukuvu, tukasema pengine sio haki sisi wataalam na sekta binafsi na wadau kwanini tusifanya jambo tukutane na tuongee kuhusu hii kitu.”

Mkurugenzi huyo wa TPSF amesema, uelewa juu ya changamoto hiyo ni muhimu, kwa kuwa kama haitatatuliwa, mahindi ya Tanzania yatakosa soko, kitendo kitakachoathiri uchumi wa wakulima.

“Hii biashara ya mahindi ni kubwa, lakini ukiichezea hutapata biashara na utapoteza maisha ya watu. Watu wakigundua mahindi ya Tanzania yana sumu kuvu, hautapata soko. Ifike wakati mkulima awe na ujasiri wa kulima kwa kuwa na uhakika wa kuvuna mahindi na kuyasafirisha,” amesema Nanai.

Naye, Mkurugenzi wa Idara Usalama wa chakula katika Wizara ya Kilimo, Honest Kessy, amesema kilimo cha mahindi kimekuwa na changamoto ikiwemo, kuuza bidhaa bila madaraja.

“Tuna changamoto ya kutokuwa na mbegu aina moja, unakuta katika gunia moja kuna mbegu hata tano, lakini ukichukua kutoka zambia unakuta aina moja, hivyo hatuwezi kusema tunauza mahindi ya aina gani,”

“Tatizo lingine kubwa lililojitokeza sasa hivi ni uchafuzi wa sumu kuvu, moja ya juhudi zinazofanywa ni mradi wa kitaifa wa kudhibti uchafuzi wa sumukuvu, malengo makubwa ni kuongeza uelewa juu ya tatizo la uchafunzi wa sumu kuvu. Kwa pamoja tukiweka nguvu tutafanikiwa,”  amesema Kessy.

Kessy amesema changamoto hizo zinasabisha mahindi ya Tanzania kutokidhi viwango vya ubora na usalama wa  kikanda na kimataifa, jambo ambalo limesababisha kuuzwa kwa bei ndogo na hata kukataliwa kwenye masoko.

“Sote tunakumbuka, tarehe 5 Machi 2021 tulipata katazo kutoka Kenya na Burundi kwamba mahindi yetu yana kiwango kikubwa cha sumukuvu na ukiangalia sisi kama watanzania, wote tulipoteza kuanzia mfanyabiashara, mkulima hadi msafirishaji.

“Na leo hii tuko hapa kujadili tufanye nini tuweze kuwa na njia endelevu yam azo yetu kuaminika ili yoyote akisema mahindi aambiwe nenda Tanzania na naamini kwa umoja wetu tutapata suluhishola changamoto hii.” amesema Kessy.

Kessy amesema, takwimu zinaonyesha katika kipindi cha miaka mitano mfululizo kumekuwa na ongezeko la uzalishaji wa mazao,  ambapo kwa mwaka 2020/2021, zimezalishwa tani milioni 6.7.

Kessy amesema, tafiti zinaonyesha zao la mahindi linachukua karibu asilimia 9 ya mazao yanayozalishwa Tanzania, na kufanya liwe zao la kwanza kwa umuhimu kama zao la chakula na biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Amesema soko kuu la mahindi ya Tanzania ni Kenya, ambapo hupeleka  tani 72,460 kila mwaka sawa na asilimia  70 ,  ya mahindi yote yanayouzwa nje ya nchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Ndege ya Precision Air yaahirisha safari kwa hitilafu, nyingine yatua kwa dharura

Spread the love  NDEGE ya Shirika la Precision Air imeshindwa kufanya safari...

Habari Mchanganyiko

NMB yakabidhi vifaa tiba hospitali Mtwara  

Spread the loveBENKI ya NMB Kanda ya Kusini imetoa msaada wa vifaa...

Habari Mchanganyiko

Kasilda Mgeni anasisitiza umoja, ushirikiano Same 

Spread the love  MKUU mpya wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda...

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

error: Content is protected !!