September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sakata la Zitto, Prof. Assad, Rais Magufuli laanza kufukuta kortini

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo

Spread the love

HATUA za awali katika kesi iliyofunguliwa na Zitto Kabwe, kupinga hatua ya Rais John Magufuli kumteua Charles Kichere, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), zimeanza kuchukuliwa. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea).

Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam leo tarehe 28 Januari 2020, uendeshaji wa kesi hiyo namba 1/2020 umeanza ambapo taratibu za awali zimechukuliwa.

Zitto ambaye ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, amefungua kesi hiyo dhidi ya Rais John Magufuli, Prof. Adelardus Kilangi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Profesa Mussa Assad, CAG mstaafu.

Kwenye kesi hiyo, Zitto anapinga sheria mpya ya Ukaguzi ya Taifa Namba 11/2008, iliyoweka awamu mbili za mtu kuongoza ofisi ya CAG.

Lakini pia, Zitto kupitia kesi hiyo anatuhumu uamuzi wa Rais Magufuli kumuondoa Prof. Assad madarakani kabla ya muda wake kisheria kutimia.

Zitto anawakilishwa na wakili wake Nyaronyo Kicheere, wakati Jamhuri ikiwakilishwa na mawakili wanne wakiongozwa na Gabriel Malata ambapo Prof. Assad akiwakilishwa na wakili Ambros Mkwera.

Majaji wanaosimia kesi hiyo ni Jaji Juliana Masabo, Jaji Lameck Mlacha (kiongozi) na Jaji Benhajj Masoud. Kesi hiyo imeahirishwa mpaka tarehe 18 Februari 2020, itakapotajwa

error: Content is protected !!