Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa SAKATA LA WARAKA: Lusinde amgwaya Membe 
Habari za SiasaTangulizi

SAKATA LA WARAKA: Lusinde amgwaya Membe 

Spread the love

MBUNGE wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde, maarufu kwa jina la Kibajaji, “ameshindwa” kufanya kazi aliyotumwa. Anadaiwa alipangwa kumshambulia kwa njia ya kumvunjia heshima, aliyekuwa waziri wa mambo ya nchi za nje na uhusiano wa kimataifa, Bernard Membe. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari, leo Jumamosi jijini Dar es Salaam, Lusinde alisema, “…ninamuweka kiporo Membe. Nitamjadili siku nyingine.”

Alisema, “…ninaenda safari nchini China. Nina ziara ya kazi ya kibunge, nikirudi nitamshughulikia Membe. Nitamkuna panapo muwasha. Yule Bernard Membe, hana lolote.” 

Kauli ya Lusinde kuwa anamuweka kiporo Membe, imekuja muda mfupi baada ya mwanadipromasia huyo mashuhuri nchini kuandika katika ukurasa wake wa twitter, kuwa Lusinde amepanga kumchafua.

Katika andishi lake, Membe alisema, “Ndugu yangu Kibajaji Lusinde, safiri salama na urejee salama, ili utekeleze maagizo uliyopewa ya kunishambulia. Niguse, ninuke!”

Jina la Membe, limekuwa likitajwa kwa kasi katika siku za hivi karibuni, kufuatia madai kuwa mwanasiasa huyo aliyetumikia nafasi ya waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa, kwa miaka minane wakati wa utawala wa Jakaya Mrisho Kikwete, amepanga kujitosa katika mbio za urais mwaka 2020 kupitia CCM.

Pamoja na kwamba Membe mwenyewe hajaweka wazi jambo hilo, lakini watu waliokaribu naye wanasema, “liwe jua au inyeshe mvua,” ni lazima atajitosa katika kinyanganyiro hicho.

Baadhi ya wachambuzi wa kisiasa wanasema, ukimya wa Membe kuhusu urais wa 2020, ndiyo chanzo kikuu cha kushambuliwa kwake na makundi mbalimbali yanayojinasibu kuwa “watetezi wa Rais Magufuli.”

Katika mkutano wake wa leo, Lusinde alisema, anafurahia kazi inayofanywa na Cyprian Musiba ya kutukana viongozi wakuu wastaafu, kwa sababu wao ndio waanzilishi wa utaratibu wa kutukana viongozi wastaafu.

Anasema, “mimi nafurahia Musiba kutukana viongozi wastaafu, sababu Kinana alitukana viongozi wake akawaita mizigo. Nape amepata umashuhuli kwa ajili ya matusi. Nashangaa wanapokasirika. Huu utarudi wameutengeneza wao wenyewe.”

Anasema, “kitendo wanacholalamikia hakina uhalali, kwa sababu wao ndio waanzilishi. Wasiwe na pande mbili, wanashughulikiwa wao wanapanda juu.”

Lusinde amedai kuwa malalamiko ya viongozi hao wastaafu yanatokana na kitendo cha Rais Magufuli kuziba mianya yao ya upigaji ndani ya CCM na serikali.

Amesema, Kinana na Makamba, wamejifedhehesha kumjibu Musiba kupitia waraka huo. Kwa maoni yake, walipaswa kuwatumia vijana kumjibu.

Hata hivyo, Lusinde ameshindwa kujibu madai kuwa kwa kauli yake hiyo, haiwezekani kuwa naye ametumwa na wanaotajwa kwenye waraka wa Kinana na Makamba.

“Waraka wa hovyo, hauna maana yoyote. Wao ndio waliuanzisha. Walikuwa wana vijana wao wanawatuma kutukana watu. Ukitengeneza utaratibu, ujue utakugeukia. Watulie, wasikilizie sindano. Wafanye kazi za uhalali, wasifanye kazi za udalali,” ameeeleza Lusinde.

Kwa mujibu wa Lusinde, ili kuondoa mzizi wa fitina, Rais Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho taifa, aruhusu ripoti ya ukaguzi wa mali za CCM itolewe hadharani, ili umma uweze kujua namna mali hizo zilivyopigwa na wapigaji wake.

Lusinde anakuwa mtu wa saba kujitokeza kumtetea Musiba na wanaomtuma. Wengine waliojitokeza kumtetea Musiba na kuwashambulia Kinana na Makamba, ni pamoja na mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku, maarufu kwa jina la Msukuma; mbunge wa Nzega, Hussein Bashe; mbunge wa Simanjiro, James Millya na mbunge wa Busega, Dk. Raphael Chegeni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!