July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sakata la utoroshwaji wanyama hai laibuka

Wanyama wa Twiga ambao ni sehemu ya wanyama waliotoroshwa 2010

Spread the love

SAKATA la utoroshwaji wa wanyama hai katika Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) limeibuka tena bungeni baada ya Mbunge wa Viti Maalum, Christowaja Mdinda (Chadema) kuliibua. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Akiuliza swali la nyongeza, Mtinda aliitaka serikali kueleza ni kwanini mpaka sasa imeshundwa kutoa taarifa iwapo tume iliyoundwa kwenda nchini Qatar kwa ajili ya uchunguzi ilimaliza kazi hiyo?

Pia alitaka kujua wakati wa utoroshwaji huo Usalama wa Taifa ulikuwa wapi ikiwa ni pamoja na uwajibikaji wa vyombo vya ulinzi na kwamba, serikali inaweza kutekwa.

Awali katika swali la msingi la mbunge huyo, alitaka kujua serikali ina mkakati gani wa kukomesha uharamia wa utoroshwaji wa wanyama pori ili kulinda utalii.

“Hapa nchini kumekuwepo na utoroshaji wa wanyama hai wakiwemo Twiga kwenda Uarabuni. Je, serikali ina mkakati gani wa kukomesha uharamia huo ili kulinda utalii wetu?” amehoji.

Akijibu maswali hayo Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohammood Mgimwa amesema, ni kweli wanyama walitoroshwa lakini hatua za kiuchunguzi bado zinaendelea.

Amesema, utaratibu wa kamati pamoja na maofisa mbalimbali waliunda tume na kinachofanyika ni kutafuta utaratibu wa kwenda katika nchi husika ili kufanya uchunguzi wa jambo hilo.

Hata hivyo amesema, kutokana na uzito na umuhimu wa jambo hilo serikali imewafukuza kazi watumishi ambao siyo waaminifu pamoja na kuwasimanisha watumishi wapatao 15.

Amesema, serikali imeweka mikakati maalumu ikiwa ni pamoja na kuimarisha ulinzi katika viwanja vya ndege, bandarini pamoja na maeneo ya mipakani.

error: Content is protected !!