May 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Sakata la Tz Ulaya: Balozi amvaa Zitto

Jestas Nyamanga, Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imesema, haijawekewa vikwazo na kunyimwa misaada na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU), kama inavyodaiwa na baadhi ya wanasiasa na wanaharakati nchini humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa Jana tarehe 19 Novemba 2020, na Mwakailishi wa Tanzania katika Umoja wa Ulaya, Balozi Jestas Nyamanga akitoa ufafanuzi kuhusu mahusiano ya taifa hilo na EU.

Kwa mujibu wa Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT – Wazalendo kupitia katika ukurasa wake Twitter, alitoa taarifa kwamba, Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la EU imetoa azimio la kusitisha misaada kwa Tanzania.

Balozi Nyamanga taarifa kwamba taarifa hizo hazina ukweli wowote kwa kuwa, Bunge la EU halijatoa maazimio hayo.

Ufafanuzi huo umetolewa kufuatia kusambaa kwa taarifa katika mitandao ya kijamii zinazodai, kwamba Bunge la EU liemazimia kusitisha misaada pamoja na kuiwekea vizuizi Tanzania.

Kwa maelezo kwamba, mchakato wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, uligubikwa na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo

“Kwa hiyo nawaomba Watanzania puuzeni taarifa zinazoenezwa hazina ukweli,  hazina uhalisia wowote naomba niwahakikishie uhusiano wa Tanzania na Umoja wa Ulaya ni mzuri sana, kwa zaidi ya miaka 45 tumekuwa na mahusiano na EU  na kipindi chote umekuwa mzuri na kipindi hiki bado mahusiano mazuri,” amesema Balozi Nyamanga.

Zitto alidai kwamba, EU imesema haitatoatena msaada kwa Tanzania hadi pale taifa hilo litakapoimarisha misingi ya demokrasia.

Mwanasiasa huyo alidai, Tanzania na EU zilisaini mkataba wa msaada wa kuimarisha utawala bora na maendeleo wenye thamani ya Sh. 1.6 Tril. Juni 2014.

Na kwamba, mkataba huo unaisha Juni mwaka huu, hivyo umoja huo umesema, hawatauendeleza hadi masharti yao yatakapotekelezwa.

“Kwa wale wanaofuatilia, huu ndio mkataba kati ya Tanzania na EU kuhusu misaada ulisainiwa na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Juni 2014. Jumla ya msaada huo ni Euro 626, unaisha Juni 2020 na EU wamesema hawatoi tena hadi waone demokrasia inarudi nchini,” aliandika Zitto.

Hata hivyo, Balozi Nyamanga alisema, EU haijasitisha utoaji wa fedha hizo.

“Eti taarifa zinadai Bunge la EU zinaadhimia kuifutia Tanzania msaada wa Euro 626 Mil, taarifa inadai Tanzania inapewa na Umoja wa Ulaya kila mwaka, ni upotoshaji mkubwa si kweli, EU haiipi Tanzania Euro 626 Mil.  sawa na tril. 1.6,” amesema Balozi Nyamanga.

“Wanadai kuna majadiliano yanaendelea kuiwekea Tanznaia vikwazo vya kiuchumi,  si kweli hakuna majadiliano yanayoendelea katika  Bunge la Ulaya, hakuna majadiliano na azimio la Kamati ya Mambo ya Nje kuhusu kuiwekea Tanzania vikwazo na wala hakuna maazimio ya bunge kwa Tanznaia kuuza bidhaa zake katika nchi za ulaya,” amesema Balozi Nyamanga.

error: Content is protected !!