Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Sakata la saruji, Majaliwa awaonya mawakala, atoa maagizo 
Habari Mchanganyiko

Sakata la saruji, Majaliwa awaonya mawakala, atoa maagizo 

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu,
Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Viwanda na Biashara ikamilishe utaratibu wa kuwa na bei kikomo ya saruji ili kuuwezesha kila mkoa kujua bidhaa hiyo inapaswa kuuzwa kwa bei gani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Amesema lengo ni kuondoa upandishwaji holela unaofanywa na wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu.

Pia, ametoa onyo kwa mawakala wa saruji kutoficha bidhaa hiyo kwa lengo la kupandisha bei kwa sababu kitendo hicho ni sawa na uhujumu uchumi, hivyo watakaobainika watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria.

Majaliwa ametoa agizo hilo jana Jumatatu, tarehe 7 Desemba 2020 alipozungumza na Wakuu wa Mikoa, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Maafisa Biashara wa Mikoa, Mawakala wa saruji walioko mikoani na Wakurugenzi wa viwanda vya saruji.

Kikao hicho ambacho Majaliwa amekiongozo kwa njia ya televisheni akiwa ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma kilihusu suala la bei na mwenendo wa upatikanaji wa saruji.

Waziri mkuu amesema, lazima utaratibu wa kuwa na bei kikomo ya saruji ukamilike ili kujua kila mkoa bidhaa hiyo inapatikana kwa kiasi gani.

“Mfano saruji inazalishwa Tanga au Dar es Salaam alafu Morogoro inauzwa kwa Sh.28,000 sasa Kigoma itauzwaje lazima kuwe na bei kikomo.”

Amesema, suala hilo halihitaji kuundiwa bodi kwa sasa kwani vyombo vya kusimamia biashara vipo, wizara husika ipo, hivyo amewataka wahusika wote wahakikishe wanasimamia suala hilo kikamilifu ili kuwawezesha wananchi kupata bidhaa hiyo kwa bei nafuu.

Waziri mkuu ametumia fursa hiyo kuiagiza Tume ya Ushindani (FCC) ifanye ukaguzi ili kubaini kama bei za bidhaa hiyo ni shindani na zina tija kwa wananchi kwa sababu katika maeneo mengine hazina uhalisia na zinasababisha usumbufu nchini.

“…Mawakala badilikeni na achaneni na tabia ya kuficha bidhaa kwa ajili ya kuzipandisha bei, ukikutwa unatengeneza mazingira ya kuifanya bidhaa isipatikane kwa lengo la kuipandisha bei huo ni uhujumu uchumi.”

“Ukikamatwa na bidhaa ambayo inatafutwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yako,” amesema Majaliwa.

Pia, Majaliwa amewaagiza viongozi wa Wizara ya Viwanda na Biashara watembelee viwanda mbalimbali ili kusikiliza matatizo yanayowakabili wenye viwanda na kushirikiana nao katika kuyapatia ufumbuzi.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema licha ya bei ya saruji kuanza kupungua nchini, amewataka wakuu wa mikoa waendelee kufanya ukaguzi na kufuatilia mwenendo wa bei ya saruji ili kubaini kama bei wanayouziwa wananchi ni halali na wahakikishe bei ya bidhaa hiyo inaendelea kushuka.

Amesema viwanda vya saruji havina budi kupanua wigo kwa kuwa na mawakala wengi hadi vijijini ili kumudu kuwafikia wananchi wengi zaidi kwa sababu mahitaji ya saruji nchini ni makubwa kwani Watanzania wanaboresha makazi yao kwa kujenga nyumba bora hadi vijijini.

Licha ya bei ya saruji kuanza kushuka katika mikoa mbalimbali nchini, imeelezwa kuwa katika baadhi ya mikoa kama Dodoma, Ruvuma, Simiyu, Tabora bado upatikanaji wa bidhaa hiyo hauridhishi na inauzwa kwa bei kubwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa 12 wa kilo 726.2 za dawa za kulevya wafikishwa mahakamani

Spread the love  WATUHUMIWA watatu wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!