Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Sakata la saruji, Majaliwa atoa maagizo kwa Ma RC ‘wakamateni’
Habari Mchanganyiko

Sakata la saruji, Majaliwa atoa maagizo kwa Ma RC ‘wakamateni’

Spread the love

WAZURI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewaagiza wakuu wa mikoa (RC) yote kufanya ukaguzi kwenye viwanda vya kuzalisha saruji, mawakala, wauzaji wa kati na wadogo pamoja na kuwakamata wanaorundika bidhaa hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Ametoa agizo hilo jana Jumamosi tarehe 21 Novemba 2020 wakati akizungumza na wakuu wa mikoa yote nchini kwenye kikao alichokiendelesha kwa njia ya video kuhusu tatizo la kupanda kwa bei ya saruji nchini.

Amesema lazima serikali ichukue hatua kuhusu suala hilo kwasababu hakuna sababu yoyote ya kupandisha bei.

Bei ya Saruji imelalamikiwa kupanda kuanzia Oktoba na Novemba 2020 huku Majaliwa akieleza, bei zilikuwa za kawaida Septemba ambapo kiasi cha juu cha bei ya saruji kilikuwa Sh. 16,000 kwa mikoa ya mbali kama Kagera na Kigoma ambayo haina viwanda.

“Kwenu wakuu wa mikoa kama ambavyo mmefanya kazi ya kupita maeneo yote yenye viwanda na mawakala, endeleeni na sasa tufanye ukaguzi wa kina kwa mawakala kwenye maghala yao kama mlivyofanya kwenye sukari, ukikuta mtu amelundika saruji nyingi huyo ni wakukamata kwasababu anazuia makusudi.”

“Hatuwezi kuvumilia hali iendelee tukaiacha tu, yapo maeneo watu walikuwa wananunua saruji kwa Sh/13,000, yapo maeneo Sh.14,000, Sh.14,500, kiasi kikubwa kilikuwa ni Sh.16,000 kwa maeneo ya mbali kama Kagera ambapo hakuna viwanda, lakini sasa inapatikana kwa Sh.25,000 hilo halikubaliki hata kidogo” amesema.

Amewaeleza wakuu wa mikoa hao hakuna sababu yoyote inayopelekea kupanda kwa bei ya saruji na hata zikitolewa sababu za usafirishaji bado sio kigezo kwakuwa hata miezi iliyopita saruji ilikuwa ikisafirishwa kwenye barabara hizo hizo.

“Hakuna tozo zozote za kodi zilizoongezwa na TRA, kama kungekuwa na tozo za kodi wangeendelea kupandisha tena sio kwa kiwango hicho lakini kwakuwa hatuna ongezeko lolote la kodi hatuna sababu ya kuwa na bei kubwa kiasi hicho” amesema Majaliwa na kuongeza.

“Jambo hili halikufanywa kwa malengo mazuri, limefanywa kwa malengo mabaya ya kutaka kuleta taharuki nchini na kufanya serikali ishindwe kufanya kazi zake nyingine za maendeleo, ihangaike na saruji” amesema.

Hata hivyo, amesema serikali haiwezi kukubaliana na malengo hayo mabaya kwakuwa wanapo hamasisha ujenzi wa viwanda ili vizalishe bidhaa malengo ni bidhaa hiyo ipatikane kwa wingi na bei zake ziwe za kawaida kwasababu mzalishaji hasafirishi malighafi kutoka nje ya nchi.

Katika hatua nyingine, Majaliwa amewaagiza viongozi wa Tume ya Ushindani (FCC) kuwafuatilia wamiliki wenye viwanda vya saruji na kuwachunguza uhalali wa bei zinazopangwa na mawakala na wafanyabiashara wa saruji nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!